Saturday, September 6, 2014

NJOMBE WAASWA KATIBA MPYA

Wananchi mkoani Njombe wamekuwa na mtazamo tofauti juu ya bunge la katiba linaloendelea mkoni Dodoma kufuatia kundi la baadhi ya wajumbe ukawa kugoma kuendelea kuhudhuria huku wakielekeza mitazamo yao kwa kumshauri raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzani dokta jakaya kikwete kusitisha bunge hilo kwa madai kuwa bunge hilo halina usawa
Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara mjini Njombe uliowakutanissha na  kituo cha sheria na Haki za Binadamu mjini Njombe wananchi hao wamesema wanashangazwa kuona bunge hilo linaendelea huku wajumbe wengine wakiwa hawapo bungeni kwa kuwa katiba si ya wachache bali ni ya watanzania wote kama anavyoeleza  Joyce Chumi mkazi wa Njombe mjini
Akizungumza kwenye mkutano huo mwenyekiti wa chama cha TLP mkoani Njombe bw Erasto Mponji amewaomba wajumbe wa haki za binadamu kumshauri raaisi ili aweze kuwasikiliza wajumbe waligoma kuedelea na bunge nili katiba iliyokusudiwa ipatikane

Awali akizungumza na mamia ya wananchi waliohudhuria kwenye mkutano huo wakili wa kituo cha sheria na haki za binadamu Bw Elibariki Maeda amewataka wananchi hao kusoma rasimu ya katiba  pamoja na kufuatilia vyombo vya habari ili iliwajue kama kinachojadiliwa bungeni ndio kile walicho kitoa kwenye tume ya jaji walioba

Kamati hiyo ya kituo cha sheria haki za binadamu pia imewataka wananchi mkoani humo kujiandaa na rasimu ya pili na wajitokeze kutoa maoni yao pindi watakapo hitajika pamoja na kwataka wananchi kuacha tabia ya ukatili wa kijisia hasa wanawake na watoto

No comments:

Post a Comment