Wadau mbalimbali wameanza kujitokeza kutoa michango yao katika shule ya sekondari ya wasichana Utweve iliyoko kata ya Ukwama wilayani Makete inayotarajiwa kufunguliwa rasmi mwakani
Akizungumza namtandao huua mtendaji wa kijiji cha Utweve Bw.Method Sanga amesema kuwa baada ya siku chache kutembelewa na katibu mkuu wa CCM Taifa Ndugu.Abdurahan Kinana ambapo waliahidiwa kupowa bati 200 ikiwa ilikabidhiwa mifuko ya saruji 100 kutoka kwa Msamalia mwema anajulikana kwa jina la Titho
Amesema kuwa kuanzia kipindi hicho wadau wameanza kutoa michango mbalimbali ktk shule hiyo ili ifikapo mwaka 2014 wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali waanze masomo shuleni hapo
Shule hiyo yenye jumla ya madarasa 7 nyumba ya mwalimu 1 ikiwa siku ya jana mkuu wa wilaya ya Makete Mh.Josephine Matiro kuangalia maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo ambapo amewaagiza kuanza mapema ujenzi wa vyoo ili pindi wanafunzi wanapoanza iwe rahisi kuishi katika mazingira safi na salama
Hata hivyo Bw.Sanga amewataka wazawa wa makete ambao wanaishi nje ya wilaya wawe ni watu wa kuipenda makete yao kwa kusaidia katika mambo ya kijamii ambapo amesema hivi sasa wadau ambao wameanza kutoa michango hiyo ni wazawa kutoka kijiji cha Mang’oto,maliwa,Usagatikwa na sehemu zingine
Aidha amemshukuru mkuu wa wilaya ya Makete kwa kuwasaidia katika kuendeleza ujenzi huo na kuwatembelea mara kwa mara na amesema huo ni mfano katika uongozi wa kuigwa

No comments:
Post a Comment