Monday, December 16, 2013

MAKETE WANAHABARI WAASWA KUWA WELEDI




Waandishi wa habari wameaswa kufuata maadili ya taaluma yao ili kutoviingiza vyombo vya habari ktk matatizo na kuipotosha jamii

Wito huo umetolewa hii leo na M/kiti wa halmashauri ya wilaya ya makete Mh.Daniel Okoka aliyekuwa mgeni rasmi wakati akifungua mafunzo ya kuijengea uwezo bodo ya redio kitulo fm pamoja na wakuu wa Idara kwa ufadhili wa mfuko wa kusaidia vyombo vya habari nchini Tanzania Media Fund(TMF) mafunzo hayo yatakayochukua siku 5 kuanzia leo hadi ijumaa ya tarehe 21 disemba mwaka huu

Ktk mafunzo hayo yalihodhuriwa na wanahabari kutoka kitulo fm redio,bodi ya redio na muwezeshaji Dr.Alfred Rwechengula ktk kuhakikisha redio inaingiza kiasi kikubwa cha  mapato kwa njia ya uboreshaji wa vipindi vyenye kuelimisha jamii

Jumla ya wanahabari 10 wameanza kupata mafunzo hayo ili kuelimisha jamii ya wanamakete na nje ya makete pia ili kuongeza uelewa kwa wanajamii hasa ktk Nyanja ya Elimu,Afya,Mazingira pamoja na Biashara

Redio kitulo fm ambayo ilianzishwa mwaka 2005 kwa msaada wa UNICEF kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Makete Mh.Okoka ametaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kuwa ni pamoja na wananchi kupata habari za Makete na duniani kwa ujumla kwa wakati muafaka,kuwahamasisha vijana kujishughulisha na maendeleo ktk jamii,imetoa ajira kwa vijana wenye taaluma ya uandishi wa habari na Utangazaji,imesaidia kutangaza matangazo ya halmashauri na kuwafikia walengwa kwa wakati

Hata hivyo amezitaja baadhi ya changamoto ambazo redio inakumbana nazo kuwa ni pamoja na vifaa duni hivyo kutofikia baadhi ya maeneo hata katika wilaya ya makete,kituo kinaingiza mapato kidogo pamoja na kuwa na idadi ndogo ya wanahabari waliopo kituoni hapa

No comments:

Post a Comment