MSANII
wa maigizo na filamu, Coletha Raymond ‘Koleta’ amefunguka na kutoboa
siri ya moyoni juu ya chanzo cha kuwachukia wanaume huku akisisitiza
kuendelea kuwa peke yake na kuifanya pombe ndiyo faraja kubwa.
Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu mwanzoni mwa wiki hii,
Koleta alisema kamwe hawezi kusahau maumivu aliyopewa na mchumba wake
wa zamani baada ya kumfuma zaidi ya mara moja na kumsababishia maumivu
makali moyoni.
“Niliumia sana, unajua nilikuwa bado binti hivyo nilimpenda kwa moyo
wangu wote, alikuwa akiniambia maneno mengi mazuri na matamu lakini
mwisho wa siku nikaishia kuumia,” alisema Koleta.


No comments:
Post a Comment