| Mheshimiwa Bonnah Kaluwa akihojiwa na mwasisi wa blog ya Mahabati Upendo Martin Mwase |
Mheshimiwa Kaluwa alisema idadi kubwa ya watoto wanaofanya vizuri
wanatokea katika familia masikini, ambazo hazina uwezo wa kuwalipia ada
watoto hao, hali inayowakwamisha watoto hao katika elimu ya sekodnari.
Alisema hayo wakati akifanya mahojiano maalumu na Blog ya mahabati katika hotel ya Serena iliyopo Posta jijini Dar es salaam.
Aidha alisema moja ya changamto kubwa iliyopo katika elimu, ni uwezo
mdogo wa baadhi ya familia ambazo watoto wanaofaulu wanatokea.
“mimi naumia sana kuona watoto wenye uwezo mkubwa wa elimu wakiwa wanashindwa kuendelea na elimu kwa sababu ya kukosa ada ambayo ni elfu 40 tu kwa mwaka, na ndiyo maana nimeamua sasa kuanzisha mfuko wa kuwasaidia watoto hao.
“kwa kuanza nimeanza na watoto mia moja ingawa watoto wako wengi ila mimi nimeamua nianze na hao, nimejaribu kuomba ufadhili katika kampuni zaidi ya 90, kamupuni 40 zimeonyesha moyo wa kunisaidia katika jitihada zangu hizi.
“kampuni ya simu za mikononi Tanzania Tigo imekubali kuwasomesha watoto zaidi ya 40, na mimi mwenyewe nasomesha watoto wengine watano kwa kushirikiana na Rafiki zangu”alisema Mheshimiwa Bonnah Kaluwa.
Hata hivyo aliongeza kuwa tatizo hilo ni la nchi nzima, ila kwa kuwanza yeye ameamua kuanza kwa manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam.
Pamoja na mambo mengine aliwataka wanawake kujishughulisha na shughuli mbalimbali za maendeleao ili kujikwamua na umaskini.
Mheshimiwa Kaluwa ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Radio Mlimani, juu ya changamoto zinazowakabili wanawake.
Amesema kuwa pamoja na changamoto mbalimbali wanawake wanapaswa kujiamini, na kwamba wanawake wanaweza kufikia asilimia 50 katika uongozi endapo watajiamini katika nafasi mablimbali wanazopewa kwenye jamii.

No comments:
Post a Comment