Thursday, May 2, 2013

WASOMI WA CHADEMA WAJIPANGA KUWANG`OA LUKUVI,WASSIRA

a


Wanafunzi 16 wa vyuo vikuu vya mkoani Morogoro, wametangaza nia yao ya kuwania nafasi za uongozi wa kisiasa ukiwamo ubunge katika majimbo ya vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu ujao.

Wasomi hao wakiwa na kauli mbiu ya: 'Epuka utawala wa kifalume na mabavu, chagua kasi ya maendeleo,' wametangaza nia zao za kugombea nafasi hizo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Kwa kuanzia, tayari wameanza kuwahamasisha wenzao kugombea nafasi katika uchaguzi wa serikali mitaa na kata unaotarajia kufanyika mwakani.

Wasomi hao walitangaza nia hiyo katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Wanafunzi vyuoni  (Chaso)kupitia Chadema mkoani hapa.

Waliyataja baadhi ya majimbo wanayokusudia kuyavamia kuwa ni pamoja na la Isimani mkoani Iringa linaloshikiliwa na William Lukuvi, Bunda ambalo mbunge wake wa sasa ni Steven Wassira na (Rorya) mkoani Mara linaloshikiliwa na Lameck Airo.

Majimbo mengine ni Gairo mkoani Morogoro linaloshikiliwa na Ahmed Shabiby, Handeni  ambalo mbunge wake ni Dk. Abdallah Kigoda, Jimbo la Mtwara Vijijini linaloshikiliwa na Hawa Ghasia, Morogoro Mjini linaloshikiliwa na Abdulaziz Abood, Kilosa ambalo mbunge wake ni Mustafa Mkulo na Bagamoyo Dk. Shukuru Kawambwa.

Majimbo mengine ni Kigoma Mjini linaloshikiliwa na   Peter Serukamba na Newala ambalo mbunge wake kwa sasa ni George Mkuchika.

Baadhi ya wasomi hao waliotangaza nia ya kuwania ubunge na majimbo katika mabano ni Godson Kagose (Rorya), Salim Mpanda (Gairo), Omary Mvambo (Handeni) na John James (Morogoro Mjini).

Kwa nyakati tofauti, walisema wameamua kuwania nafasi hizo kwa juhudi zote na maarifa kutokana na  nchi hususani viongozi walioko madarakani kuipoteza nchi kwenye njia sahihi inayopaswa kufuatwa.

Mmoja wa wasomi hao, Omary Mvambo, kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, alidai  kuwa viongozi waliopewa dhamana hawana wazo la maisha ya walalahoi ndiyo maana wapo bungeni kisikiliza viongozi wenzao wametoa changamoto gani ili waijibu kwa matusi wakilenga kuwatisha ili wasiendelee kufichua uovu walionao.

"Tumeshuhudia utawala wa kiimla, kurithishana madaraka kama vile hakuna watu wenye uwezo wa kuongoza isipokuwa familia zao. Hili halikubaliki na tutapigana nalo hadi hapo tutakapoona usawa umeonekana," aliongeza Mvambo.

Ili kufanikisha azma yao ya kunyakua nyadhifa za uongozi hususani za kisiasa nchini, wanachuo hao waliazimia kuunda kikosi maalum walichokiita cha maangamizi kitakachowashirikisha wanachuo kutoka vyuo vyote nchini.

Wanachuo hao watakashiriki pamoja kwenye kampeni za ushawishi wa nguvu ya hoja dhidi ya utawala uliopo.

"Tunajua kuwa  wasomi hasa tunaopitia Chadema, tunapigwa vita sana. Tutakachokifanya ni kuhakikisha tunakuwa na nguvu ya pamoja na kusaidiana kupiga kampeni za nguvu na tunashinda," alisema Mva

No comments:

Post a Comment