Thursday, May 9, 2013

VIOJANA MAKETE WANADANGANYWA NA WAZAZI WAO



MAKETE
Wazazi na walezi wameonekana kuwa ni shinikizo kubwa kwa watoto kutoendelea na masomo Wilayani makete hasa kwa wale wanaolelewa na asasi ya Iringa Development of Youth Disabled and Children Care [IDYDC]shirika linalofadhiliwa na SWEDEN,ERTKSHAPEN


Hayo yalibainishwa Jana na mratibu wa IDYDC Wilayani ya makete  Hapa Bw. Godfrey Mwauta wakati akizungumza waandishi wa habari ofisini kwake na kusema kuwa wanachangamoto kubwa kwa malezi ya watoto hao kwani vitendo vya kurubuni wanafunzi vinazidi kuongezeka siku hadi siku.

Bw Mwauta alizitaja baadhi ya changamoto ambazo wanakabiliana nazo wakati wakiwalea watoto hao kuwa ni pamoja na upungufu wa chakula ukilinganisha na idadi ya watoto hao kutomaliza masomo yao kwani wakielekea likizo baadhi yao huwa hawarudi tena ili kuendelea na masomo

Bw. mwauta aliwataka wazazi wilayani makete kutoa ushirikiano wa kuwaleta kituoni watoto ili kuendelea na masomo kwani wanawajengea maisha yao ya baadaye na sio kuwalaghai na kuwaharibia maisha watoto   hao wanaolelewa katika asasi ya IDYDC

Mbali na hilo amewaasa wanafunzi wenyewe kujitambua na kukazania elimu kwa kuwataka kutoa taarifa kwa watu wanaowaamini pindi wanapokutana na vitendo hivyo vya kurubuniwa kisha kuacha shule  na kusahau wametoka katika mazingira ya aina gani.kabisa,pia kuacha kwenda sehemu za starehe kama vilabu na gest badala yake wajikite katika masomo zaidi ili waone matunda ya elimu zao baada ya kumaliza shule. 
‘’Watu wazima mnatakiwa kuwahamasisha wanafunzi katika kupata elimu zaidi na sio kuwahamasisha kufanya ngono kwani motto wa mwenzio ni mwanao na kwa yeyote atakaye kamatwa anaanafanya vitendo hivyo atachukuliwa hatua za kisheria bw.mwautwa alisema’’

Hata hivyo bw.Mwautwa alisema wamejipanga kuongeza fani mbalimbali za kuwajengea maisha mazuri watoto hao kwani fani zinazofundishwa katika asasi hiyo ni chache ambazo ni pamoja na uselemara,uashi na ushonaji kwa watoto wakike ambazo fani hizo haziwezi kukidhi mahitaji yao pindi wamalizapo masomo yao.

Pia bw.mwautwa alitaja malengo mbalimbali ya asasi hiyo ikiwa ni pamoja na kuandaa na kununua kiwanja kwaajiri ya kupata majengo ya kudumu ya kusomea wanafunzi hao pamoja na kujenga kupitia michoro mbalimbali ili kuipeleka kwa wadhamini waweze kuwasaidia katika kulimaliza tatizo la wanafunzi hao. 

Vitendo vya kurubuni watoto wilayani makete vinatokana na wazazi au walezi wa watoto hao kutowalea kwa maadili yanayofaa kwani imeonekana wazazi ndo chanzo cha kupokea pesa za mahali au ng’ombe ili kuwauza watoto wao pindi wanapoona motto amekuwa na kusahau kuwa elimu ndo msingi wa maisha yao.





No comments:

Post a Comment