WIZARA YA NISHATI NA MADINI
SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI TANZANIA
TAARIFA KWA WATANZANIA
NAMNA MIKOA YA MTWARA NA LINDI INAVYONUFAIKA NA UTAFUTAJI NA UENDELEZAJI WA GESI ASILIA

1.0 UTANGULIZI

Gesi asilia iligunduliwa kwa mara ya kwanza hapa nchini Mwaka 1974 kwenye Kisiwa cha Songo Songo, Mkoani Lindi. Ugunduzi mwingine umefanyiaka katika maeneo ya Mtwara Vijijini (Mnazi Bay-1982 na Ntorya-2012), Mkuranga (Pwani, 2007) na Kiliwani (Lindi, 2008). Kiasi cha gesi asilia iliyogunduliwa katika maeneo haya inakadiriwa kuwa futi za ujazo trilioni 8. Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kumekuwa na kasi kubwa ya utafutaji mafuta na gesi asilia uliojikita zaidi kwenye maji ya kina kirefu cha bahari. Kiasi cha gesi asilia iliyogunduliwa katika kina kirefu cha maji ni takribani futi za ujazo trilioni 33.7. Jumla ya gesi asilia iliyogunduliwa nchi kavu na baharini inafikia takribani futi za ujazo trilioni 41.7.

Rasilimali hii ya gesi asilia inaweza kutumika katika maeneo mbalimbali yakiwemo; kuzalisha umeme, malighali ya kuzalishia mbolea na kemikali, nishati viwandani, majumbuni na kwenye taasisi mbali mbali. Pia gesi asilia inatumika kama nishati ya kuendeshea magari.

FAIDA YA GESI ASILIA MKOA WA LINDI
1. Mradi wa gesi asilia wa Songo Songo- LINDI
(i) Kodi ya Huduma (Service Levy):

Songo Songo huzalisha gesi asilia takribani futi za ujazo milioni 102 kwa siku na kuletwa Dar es Salaam kwa ajili ya kufua umeme na kutumika viwandani. Kufuatana na kodi ya huduma (Service levy) Halmashauri ya Lindi inapata asilimia 0.3 ya mauzo ya gesi hiyo. Toka mwaka 2004 wakati mradi wa Songo Songo Songo ulipoanza kuzalisha gesi hadi kufikia mwisho wa 2012, Halmashauri imepata jumla ya Shs. 885 milioni. Wastani wa mapato kwa kila miezi mitatu ni Shillingi 110 millioni.

(ii) Umeme:
  • Wananchi wa Kisiwa cha Songo Songo hupata umeme wa uhakika na bure.
  • Mara tu Bomba la Gesi litokalo Songo Songo likifika nchi kavu sehemu ya Somanga Fungu, Serikali imefunga mitambo ya kufua umeme. Umeme unaofuliwa Somanga Fungu ni MW 7.5 unaotumika ni takribani MW 2.5. Umeme huu wa ziada unatoa fursa kwa viwanda kujengwa katika mkoa wa Lindi.


(iii) Maji Safi:
  • Mradi unatoa maji safi kwa wakazi wa Songo Songo kwa kuhudumia kisima cha Kijiji.


(iv) Huduma za jamii:
  • Kila mwaka wanafunzi kumi bora waliofaulu wanafadhiliwa na mradi kwenda shule ya Sekondari ya Makongo. Wanafunzi hawa wanaofaulu vizuri watafadhiliwa hadi vyuo vikuu.
  • PanAfrican (PAT) wamejenga Shule ya chekechea Songo Songo na watoto wanahudumiwa na kampuni hiyo.
  • PAT wamepeleka waalimu wawili wa chekechea katika mafunzo ya muda mrefu.
  • Zahanati ya Songo Songo imekarabatiwa na kuongeza baadhi ya vifaa.
  • Bweni la wasichana limejengwa na kuikarabati Shule ya Sekondari ya Songo Songo.
  • Ajira hutolewa kwa wakazi wa kijiji cha Songo Songo.


Huduma hizi za jamii zimegahrimiwa kwa kiasi cha Shilingi milioni 730 ($455,000) kwa kipindi cha 2004 hadi Desemba 2012.

2. Manufa kutokana Kampuni ya Maurel and Prom.