Mapigano makali yanaedelea nchini Nigeria kati ya Jeshi la Nigeria na
wapaiganaji wa kundi la Boko Haram,ikiwa ni siku ya tano toka Jeshi la
Nigeria kufanya operesheni ya kupambana na Boko haram mji wa Maiduguri
Mji muhimu wa kaskazini mashariki mwa Nigeri,Maiduguri ulifungwa na
kufanya usafiri kuwa mgumu baada ya jeshi la Nigeria kuendesha
opareshini ya masaa 24 ya kupambana na wapiganaji wa kundi la Boko
Haram.
Msemaji wa jeshi la Nigeria General Brigadier Chris Olukolade amesema
kuwa katika operesheni hiyo jumla ya waasi 17 wa Boko Haram wameuawa na
wanajeshi watatu wa jeshi la Nigeria pia wameuawa. Kufuatia maelezo
yaliotolewa na jeshi la Nigeria katika miji mitatu,Jeshi hilo limesema
kampeni hiyo inalenga kupambana na kundi la Boko Harm ambalo linataka
kusimamisha utawala wa kiisalamu Kaskazini mwa Nigeria.
Jeshi la Nigeria
limengaza kuwasemehe wapiganaji wa Boko haram watakaojisalimisha.
Katika mji wa Adamawa,wanajeshi 150 walimwaga na wengine 100 ambao
hawakutarajiwa na kuharibu kambi kaddhaa karibu na mji wa Borno.
Rais wa
Nigeria Goodluck Jonathan alitangaza hali ya hatari juma lililopita
katika miji ya Borno Yobe na Adamawa.
Katika maelezo yake Rais Goodluck
Jonathan amewataka wapiaganaji wa kundi la Boko Haram kuweka silaha
chini na kuchukua hatua ya kujisalimisha,wakati ambapo akiandaa kamati
ya kuangalia uwezekano wa kujisalimisha wapiganaji hao .
Boko Haram bado inashikilia msimamo wake.
Kwa upande wake kiongozi wa kundi la Bokoharam Abubakar Shekau
amekataa wito wa Rais Goodluck Jonathan wa kujisalimisha wapiganaji wa
kundi la Boko Haram.
Msamaha kama huo kwa wapiganaji wa kundi la Boko haram ulisaidia
kumaliza mapiagano katika eneo la Niger Delta mwaka 2009 baada ya
mapigano ambayo yalisimamaisha shughuli ya uchimbaji mafuta kwa kadhaa.
Wachambuzi wana hofu kuwa huenda hatua ya jeshi la Nigeria kufanya
opareshini hiyo dhidi ya wapiganaji wa kundi la Boko Haram,ikakwamisha
suluhisho la kisiasa la kumaliza mapigano kati ya serikali na kundi la
Boko Haram.
Watetezi wa haki za binadamu wanasema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa
ukiukaji wa haki za binadam katika opareshini hiyo.Mawasiliano ya simu
yamekatwa katika miji ya mashariki ya Kaskazini mwa Nigeria kuzuwia
wapiganji wa Boko Haram kuwasliana.
Mapigano kati ya serikali na Boko Haram yamegharimu maisha ya zaidi ya
watu 3,600 yakiwemo mauaji yaliofanywa na vyombo vya usalama tangu mwaka
2009
Mwandishi: Hashimu Gulana/ AFP
Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman
No comments:
Post a Comment