Wananchi wilayani makete
wameshauriwa kutoingia nakuvuna miti ambayo ni mali halmashauri ya wilaya
makete
Hatua hiyo imekuja baada ya kubainika kuwa
mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Efrahim mbilinyi mkazi wa iwawa kuanza
kuvuna miti katika mistu wa Iwawa plantetion mali ya halimashauri ya wilaya ya
Makete kinyume cha sheria .ambapo amekili kuvuna miti hiyo ambayo aliuziwana na
mtu aliyetambulika kwa jina moja la Sestar mkaziwa iwawa
Akitoa rai hiyo afisa mali asili na mazingira bwana Uhuru Mwembe amesema kuwa
nikosa kuvuna misitu ya halmashauri bila idhini ya idara husika.
Katika hatua nyingine bwana Mwembe
amewataka wananchi kutovuna miti michanga kwaajili ya kujengea nyumba kwani miti
hiyo sio imara na uhatarisha uimara wa nyumba kwani miti hiyo inakuwa bado
kukomaa.
No comments:
Post a Comment