Abiria zaidi ya watano waliokuwa wakisafiri na basi la kampuni ya Taqwa kutoka jijini Dar es Salaam kwenda nchini Malawi wamekufa papo hapo na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa katika ajali iliyotokea jioni hii (May 04,2013) katika eneo la Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Moja
kati ya ajali ya basi la Taqwa
(picha na maktaba yetu) |
Abiria zaidi
ya watano waliokuwa wakisafiri na basi la kampuni ya Taqwa lenye namba za
usajili T 273 CDR kutoka jijini Dar es Salaam kwenda nchini Malawi wamekufa
papo hapo na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa vibaya katika ajali iliyotokea
jioni hii (May 04,2013) katika eneo la Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Akizungumza
na mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com mmoja kati ya mashuhuda
aliyejitambulisha kwa jina la Dkt Matatala alisema kuwa ajali hiyo imetokea muda
wa saa 11 jioni wakati basi hilo likitokea mkoani Dar es Salaam kwenda nchini
Malawi.
Alisema kuwa
chanzo cha ajali hiyo ni lori lenye namba za usajili T 104 DZZ ambalo lilikuwa
likitokea Makambako kuelekea Iringa, lililokuwa likijaribu kulipita lori lenye
namba za usajili T 227 AVC na kushindwa kupita na kuishia kugongana uso kwa uso
na basi hilo ambalo pia lilikuwa likija kwa mwendo wa kasi.
Kwa mujibu
wa mashuhuda wa ajali hiyo wamesema kuwa ajali hiyo imetokea katikati ya mji wa
Nyololo ambapo ni jirani kabisa na eneo lenye matuta ya kuzuia magari kwenda
kwa mwendo kasi.
Basi la Taqwa |
Alisema
kuwa hadi majira ya saa 12.45 jioni maiti tano zilikuwa zimetolewa katika basi
hilo la Taqwa na kuwa jitihada za wasamaria wema kutoa maiti na majeruhi katika
eneo hilo zimeendelea kufanyika.
Mbali ya
maiti hizo pia alisema jumla ya majeruhi 20 waliokolewa na kukimbizwa katika
Hospitali ya wilaya ya Mufindi kwa matibabu zaidi. Dkt Matatala alisema kuwa
katika tukio hilo wananchi wameweza kuimarisha ulinzi zaidi katika eneo hilo
ikiwa ni pamoja na kulinda mali za majeruhi na abiria waliopoteza maisha yao
kwa ajili hiyo.
Wakati huo
huo wananchi wa eneo hilo la Nyololo wameelekeza lawama zao kwa jeshi la polisi
wilayani Mufindi kwa kuchelewa kufika katika eneo la tukio na kuwa taarifa
wamepewa mapema ila hadi majira ya saa 12.50 hakukuwepo na askari aliyefika
eneo hilo.
Hii ni ajali
ya pili kutokea katika wilaya ya Mufindi kwa kipindi cha wiki moja baada ya
ajali nyingine mbaya kama hii kutokea eneo la Mafinga kwa gari ndogo iliyokuwa
ikiendeshwa na paroko wa kanisa katoliki Ifunda marehemu Alfonce Mhamilawa
kutokea kwa kuingia nyuma ya lori.
No comments:
Post a Comment