Tuesday, April 2, 2013

WALIO MUUWA MWANAMKE KAGERA WAKAMATWA

Jeshi la Polisi mkoani  Kagera  linawashikilia  watu watatu   wakazi wa kijiji cha  Mumilamila wilayani Ngara  kwa  tuhuma  za mauaji  ya mwanamke mmoja  aliyeuwawa kwa  kupigwa fimbo na kisha kunyongwa shingo hadi kufa. 


Kamanda  wa polisi  mkoani kagera  Bw  Philipo  Karangi  ameiambia  radio kuwa tukio hilo limetokea  March 29,2013  majira ya saa 5 usiku nyumbani  kwa marehemu  ambapo  watuhumiwa  hao walimuuwa  Bi  Gaudesia  Saimon  mwenye umri wa miaka 65  kutokana na imani za kishilikina.


Kamanda   Karangi  amewataja  watuhumiwa wanaoshikiliwa na Jeshi hilo la Polisi kuwa ni  Alex  Minani miaka 30 , Emmanuel Minani miaka 21 na  Isaya  Saimoni  miaka 41 wote wakazi wa Mumilamila  wilayani Ngara mkoani Kagera.
Aidha     amesema   watuhumiwa  hao kwa pamoja wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote  kuanzia sasa mara baada ya upelelezi kukamilika.

No comments:

Post a Comment