KUMRADHI WA PICHA UTAKAYOIONA KATIKA HABARI HII
MATUKIO ya kutisha na ya kinyama
dhidi ya watoto wadogo yameendelea kuutikisa Mkoa wa Mbeya, baada ya mwanafunzi
wa chekechea, Ayoub Agen (6) kuuwa kwa kuchinjwa mithili ya kuku na wauaji
kuondoka na kichwa chake.
Hata
hivyo wananchi wenye hasira walifanikiwa kumnasa mmoja wa watuhumiwa wa tukio
hilo, ambaye hata hivyo jina lake halikuweza kupatikana ambapo baada ya
kummbana ili aeleze sehemu walikokificha kichwa cha marehemu aligoma
hivyo kuamua kumteketeza kwa moto.
Habari
za uhakika kutoka eneo la tukio na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa kijiji cha
Ijoka katika kata ya Mpombo, wilayani Rungwe, Rafael Mwaikenda,
zinadai kuwa tukio hilo lilitokea Machi 31 majira ya saa 11:00 jioni.
Akifafanua
zaidi Mwenyekiti huyo alisema, marehemu Agen alikuwa ni mwanafunzi
wa chekechea katika shule ya msingi Lusanje kijijini hapo na kwamba alikutwa na
mauti hayo ya kikatili baada ya watu hao wasiofahamika kufanikiwa kumuiba
nyumbani kwao.
Mwaikenda
alisema mwili wa marehemu uliokotwa ukiwa umetenganishwa kichwa na
kiwiliwili huku kichwa kikiwa hakionekani hadi sasa ikiwa ni muda mfupi tu
baada ya watu hao wasiofahamika kumwiba toka nyumbani kwa wazazi wa marehemu .
Mkazi
mwingine katika kijiji hicho, Tumpale Sankemwa, alikielezea mkasa huo, alisema
baada ya wananchi kugundua mwili huo wa marehemu waliendelea kuwasaka wahusika
na wakiwa katika harakati hizo ghafla walikutana na mtu mmoja ambaye walimtilia
mashaka.
Alisema
baada ya kumfanyia mahojiano ya kina kwa kuwa alikuwa hafahamiki na mgeni
kijijini hapo, alikuwa akijibu jeuri hivyo kuwapandisha hasira wananchi jambo
lililosababisha kuanza kumshambulia na hatimaye kumuua papo hapo.
Hata
hivyo alisema wakati wananchi wakiendelea kumshushia kipigon mtu huyo licha ya
kutotaja jina lake, alikiri kuhusika katika tukio hilo kwa kueleza kuwa
waliohusika walikuwa watatu na kwamba wenzake walikuwa wameondoka.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Mbeya, Kamishina Msaidizi wa jeshi la polisi,Diwani Athumani,
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba hadi sasa kichwa cha marehemu
huyo hakijaonekana na jeshi hilo linaendelea kufanya uchungu.
CHANZO: MBEYA YETU
No comments:
Post a Comment