Monday, April 22, 2013

MAJAMBAZI WATIKISA TARIME

WAKAZI wawili wa kijiji cha Kimusi, kata ya Nyamwaga, wilayani Tarime, wamefariki dunia, kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi ambao pia walipora mifugo 120.

Waliokufa wametajwa kuwa ni Marwa Ryoba Chacha (28) na Mwita Iserema Chacha (18).
Kamanda wa Polisi Tarime na Rorya, Justus Kamugisha, alisema jana kuwa wakazi hao waliuawa na watu hao waliokadiriwa kuwa 15 yaliokuwa na bunduki ya kivita ya aina ya SMG.

Kamugisha alisema tukio hilo lilitokea juzi, baada ya wakazi hao kuvamiwa nyumbani kwao majira ya saa 9.00 jioni.
Alisema majambazi hayo yaliyoongozwa na mmoja wao aliyefahamika kwa jina la Muruga Kichore au maarufu Ndege ya Chini, kabla ya kutenda mauaji hayo waliwapora mifugo hiyo iliyokutwa malishoni.
Aliwataja wakazi walioporwa mifugo na idadi ya mifugo iliyoporwa ikiwa kwenye mabano ni Mapinde Mniko ng’ombe (3), Ryoba Mniko (ng’ombe 2 na mbuzi 8), Marwa Chacha (ng’ombe 3), Sarige Chacha (ng’ombe 2 na mbuzi 2).
Wengine ni Ngendo Wantahe (ng’ombe 2), Marwa Ryoba (ng’ombe 3), Lilo Daud (mbuzi 30) na Mwita Mapinde (mbuzi 35).
Kamugisha alisema katika tukio hilo hakuna aliyekamatwa na polisi wanaendelea na msako.

No comments:

Post a Comment