"Nani asiyejua kuwa Ngilu ana tuhuma mbele ya (kamisheni ya) kupambana na ufisadi?" alisema Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Jakoyo Midiwo.
"Nimefadhaishwa ... walisema watatupatia baraza la wasomi, lakini wametupa wanasiasa wa vyama."Wanasiasa
wa CORD walisema watapinga uteuzi wa Najib Balala na Charity Ngilu, ambao wote walishindwa kwenye uchaguzi wa useneti hapo tarehe 4 Machi, kwa mujibu wa Capital FM ya Kenya.
Balala ameteuliwa kuwa waziri wa madini na Ngilu waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya mijini."Jamii anayotokea rais ina nafasi nne na ya makamu wa rais ina tatu. Uko wapi uso wa Kenya katika hili? Pia waliiambia nchi kwamba hawataleta wanasiasa kwenye baraza la mawaziri, lakini wameleta wanasiasa wabaya zaidi," alisema Joseph Nkaissery, mjumbe wa kamati ya uteuzi ya bunge.
Kamati hiyo itafanya vikao vya siku saba za vya hadhara kuwapa raia nafasi ya kuzungumzia uteuzi wa Kenyatta wa baraza la mawaziri.
"Nitazungumza na wenzangu kwenye kamati kuyakataa majina haya, lakini kama idadi ya wingi wa wabunge itashinda, basi Wakenya watasema," alisema.

No comments:
Post a Comment