Saturday, April 27, 2013

ANGALIA SHEREHE ZA MUUNGANO HAPA

TASWIRA MBALIMBALI ZA SHEREHE ZA MIAKA 49 ya MUUNGANO UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM


Rais Jakaya Kikwete akiwapungia mamia ya wananchi waliofurika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.



Ndege za kivita zikifanya maonesho katika sherehe za Miaka 49 ya Muungano jijini Dar es salaam leo.
Zenye rangi ya njano zinazomwaga rangi za bendera za Taifa ni ndege za mafunzo na zingine za kijivu
ni za kivita.


RAIS KIKWETE APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO TOKA KWA MABALOZI WA BANGLADESH, SLOVAK, UGIRIKI NA KUWAIT



Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Bw John haule  kwa Balozi wa Bangladesh nchini Mhe Wahidur Rahman baada ya kupokea hati zake za utambulisho na kisha kufanya naye mazungumzo leo April 25, Ikulu jijini Dar es salam

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa na Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage kwa Balozi wa Kuwait  nchini Mhe Yacoub Y. Alsanad kabla ya ya kupokea hati zake za utambulisho na kisha kufanya naye mazungumzo leo April 25, Ikulu jijini Dar es salam

 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na  Balozi wa Kuwait  nchini Mhe Yacoub Y. Alsanad kabla ya ya kupokea hati zake za utambulisho na kisha kufanya naye mazungumzo leo April 25, Ikulu jijini Dar es salam. Kushoto ni Bw Abdul Rahman Al-Hashim, Meneja wa Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait aliyeongozana na Balozi huyo

No comments:

Post a Comment