Wito
umetolewa kwa wananchi kote nchini kuacha tabia ya kutoa au kupokea rushwa
kwani ni kinyume cha sheria na haki za binadamu ikiwa ni pamoja na kurudisha
nyuma maendeleo ya taifa.
Akizungumzia kuhusu tatizo la
rushwa mwezeshaji wa shirika lisilo la kiserikali linaloshughulikia haki za Binadamu
na Jinsia Ana Claire Shija amesema wananchi
wanatakiwa kudai haki zao pasipo kutoa au kupokea rushwa ili kuhakikisha
vitendo vya rushwa vinatokomezwa kabisa hapa nchini.
Akifafanua zaidi Shija amesema
watu wenye hali ngumu kimaisha hasa wajane ,walemavu ,wanawake na watoto kutokana
na kukutana na kusuasua kimaisha kuwa na
uwezo mdogo hali inayowakatisha tamaa na kutokuwa na imani kwa wanaoshughulikia
matatizo hayo kwani huwadai rushwa ili waweze kupata msaada.
Kwa upande wa washiriki katika kuitaka
serikali kutokomeza vitendo vya rushwa hapa nchini wamesema kuna haja ya
serikali kubadilisha sheria zilizozopo tangu kuanzishwa kwa mabaraza hayo ya
usuluhishi mwaka 1985 kwani zimepitwa na wakati kutokana na wananchi wengi
kutoelewa umuhimu wake.
Hata hivyo wamependekeza kuwa
wananchi wapewe elimu itakayowasaidia kutambua umuhimu wa mabaraza hayo ya mashauri
ili kupunguza kesi za migogoro ya ndoa, kazi na ardhi katika mahakama za mwanzo.
Aidha wamesema changamoto
nyingine ni vitendea kazi na mazingira magumu katika mabaraza hayo na kutopewa motisha jambo linafanya kutomalizika kwa mashauri mbalimbali.
No comments:
Post a Comment