Saturday, February 23, 2013

WANANCHI MTWARA NUSURU WAWAVAMIE WANAHABARI ,POLISI WAINGILIA KATI KUWALINDA


Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakitokea mkoani mtwara na kusindikizwa kulindwa na jeshi la police kabla ya kuvamiwa na jopu la waandamanaji lililohisiwa kutaka kuwavamia asubuhi ya leo baada ya kutoka alfajiri ya saa 11 kuwahi kupita mkoani lindi,hapa ni eneo la nje ya  mji wa lindi barabara iendao Dar.
 Wanahabari  wa  vyombo mbali mbali  nchini  wakilindwa na  polisi asubuhi ya leo mkoani Mtwara baada ya  wananchi wenye nia mbaya kutaka  kuwavamia leo nje  kidogo na mji  wa Lindi .

Habari  zilizotua  hivi  punde katika mtandao huu kutoka Mtwara  zinadai  kuwa  kundi la  wananchi  limetaka kuwavamia  wanahabari  wa  vyombo mbali mbali  waliopo kikazi mkoani humo kwa lengo la kuwapiga .

Tukio  hilo kwa  mujibu  wa  mwanahabari wetu John Kasembe  kuwa  limetokea mapema asubuhi ya  leo  wakati  wanahabari  hao  wakijiandaa kupita mkoa  wa Lindi kwenye  barabara  kuu ya Lindi - Dar es Salaam .

Kutokana na hali  hiyo ya uvunjifu wa amani polisi wa  kikosi  cha FFU  wamelazimika  kuwalinda wanahabari  hao na kufanikiwa  kupita salama.
...........HABARI KAMILI ITAKUJIA.......

No comments:

Post a Comment