Wednesday, February 6, 2013
Mkuu wa mkoa wa Njombe akizindua pikipiki hizo tayari kwa matumizi. Hizi ndio pikipiki zilizotolewa jana kwa Jeshi la polisi.
Hili ndilo jengo la usalama barabarani lililozinduliwa jana na mkuu wa mkoa wa Njombe likigharimu zaidi ya shilingi milioni 45. Kulia ni mnadhimu wa jeshi la polisi mkoa wa NJOMBE Focus Malengo katikati ni Katibu wa mkuu wa Mkoa bwana Daniel Ngalupela na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Njombe Capt.Mstaafu Asseri Msangi. RTO Njombe bwana Maro Chacha akitoa maelekezo kwa mkuu wa mkoa wa NJOMBE.
Afisa wa polisi wa wilaya ya Wanging'ombe wa usalama Barabarani.
Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Jana Limefanya Uzinduzi wa Jengo la Usalama Barabarani Pamoja na Kutoa Pikipiki Kumi na Nne Kwa maafisa Tarafa wa usalama barabarani.
Uzinduzi wa jengo hilo liligharimu shilingi milioni 47 hadi sasa kwa michang0 ya wadau mbalimbali na shilingi milioni kumi zikitoka jeshi la polisi umefanyika na mkuu wa mkoa wa Njombe Captain Mstaafu Asseri Msangi akiwa mgeni rasmi Katika kituo cha kikuu cha polisi mkoani hapa
Pamoja na mambo mengine lakini pia amekabidhi Pikipiki kumi na nne ikiwa awali zilitolewa Nne na kufanya jumla ya pikipiki 18 kwa maafisa Tarafa wa usalama barabarani kwa tarafa zote 18 za mkoa wa Njombe.
Captain Msangi amesema kuwa usafiri huo utarahisha safari za kuwafikia wananchi katika maeneo magumu hususani vijiji ambako kumekuwa na shida ya kufikika huku akiwataka kuwa waangalifu katika matumizi ya vyombo hivyo vya moto.
Tutakufa wengine kwa hizi pikipiki na lazima tutambue kuwa ajali za barabarani zilizonyingi hutokana na pikipiki"alisema Msangi".
Aliongeza"kwanza pikipiki kabla haijapandwa inakuwa imelewa na ndio maana ikisimama haiwezi kunyooka inayumbia upande hivyo wewe ni bodi na ukiongeza bia moja hutasalimika alisikika akisema Captain Msangi".
Katika hatua nyingine Msangi amemuagiza mkuu wa usalama barabarani Maro Chacha kuongeza jitihada za kutoa mafunzo kwa madereva wa pikipiki na magari ili kupunguza ajali zinazojitokeza mara kwa mara kwani ajali nyingi zinatokana na madereva wa pikipiki.
No comments:
Post a Comment