POLISI Bunda wamesema watamfikisha mahakamani wakati wowote
Ofisa tabibu mmoja wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, anayetuhumiwa
kumtoa mimba mhudumu mmoja wa baa ambaye kwa sasa hali yake ni mbaya.
Ofisa tabibu huyo Michael Musimu, ambaye amekuwa
akifanya kazi katika kituo cha afya Manyamanya, kilichoko Bunda,
anashikiliwa na polisi akituhumiwa kumtoa mimba mhudumu mmoja wa baa
ijulikanayo kwa jina la Savana, iliyoko mjini hapa.
Polisi wamemtaja mhudumu huyo kuwa ni Salome
Saimon Bugunda, ambaye sasa hali yake ni mbaya na amepelekwa katika
Hospitali ya Rufaa Bugando Mwanza kwa matibabu zaidi.
Imedaiwa kuwa tukio hilo lilitokea juzi na kwamba
baada ya Musimu kumtoa mimba mhudumu huyo, hali yake ilibadilika na
kumpeleka katika kituo cha afya Manyamanya, lakini hali yake ilizidi
kuwa mbaya zaidi na ndipo akakimbizwa katika hospitali ya DDH Bunda
ambako pia alipewa rufaa ya kwenda Bugando.
Aidha, imeelezwa kuwa mhudumu huyo ameumizwa vibaya kwani sehemu ya utumbo wake umetoka nje.
No comments:
Post a Comment