Wednesday, February 6, 2013

BIBI AMUUA MJUKUU WAKE KWA SUMU




Mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka miwili huko California amekufa baada ya bibi yake kwa bahati mbaya kumpatia dawa ya kufanyia usafi anywe, akiamini yalikuwa maji salama ya kunywa, polisi wamebainisha jana.
 
Jack Shearer alikuwa akicheza kwenye karakana ya babu yake katika Mtaa wa Childs huko Merced Ijumaa mchana.
 
Msemaji wa polisi alisema kwamba wakati mtoto huyo aliposhikwa na kiu, bibi yake alimpatia chupa aliyoiona juu sakafu ya lori la mumewe ambapo aliamini ilikuwa na maji salama ndani yake.
 
Kinyume cha matarajio kumbe chupa hiyo ilikuwa na dawa yenye nguvu mno ya kuondosha uchafu inayotumika kusafishia magurudumu ya chuma kwenye magari na mtoto huyo akaanza kupaliwa, gazeti la Merced Sun-Star linaripoti.
 
Babu wa mtoto huyo haraka akapiga simu polisi baada ya kubaini makosa hayo, lakini ikaishia kumkimbiza kwa gari hadi kituo cha afya cha Mercy.
 
Mtoto huyo kisha akasafirishwa kwenda Hospitali ya Watoto mjini Madera, ambako alitangazwa kuwa amefariki dunia.
 
Mamlaka zinajipanga kufanya uchunguzi na ukaguzi wa mwili huo, lakini hakuna mashitaka yoyoye yanayotarajiwa kufunguliwa kwa sasa. Wapelelezi wanaamini kifo hicho hakina chochote cha zaidi ya ajali ya kawaida tu.
Majina ya wazazi wa mtoto huyo hayakuwekwa bayana.

No comments:

Post a Comment