Shocking: Paolo Berlusco
MSHAMBULIAJI
Mario Balotelli anajikuta katika wakati mgumu tena kwenye maiaha yake
ya soka, baada ya kuitwa nyani mdogo na kaka wa mmiliki wa AC Milan,
Silvio Berlusconi.
Bosi
wa gazeti, Paolo Berlusconi, mwenye umri wa miaka 64, alifanya ishara
ya kushitusha dhidi ya Balotelli, mwenye umri wa miaka 22, kiasi cha saa
kadhaa kabla ya mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City kuichezea
mechi yake ya kwanza AC Milan kufuatia kurejea Italia.
Berlusconi
alikuwa amehudhuria mbio za FabrizioSala, mgombea mwenza wa kaka yake
katika chama cha People of Freedom, wakati alipotoa maneno hayo na
kupokedwa kwa kicheko na watu.
Baada
ya kutoa maneno ya utani kwa Nahodha wa Costa Concordia, Francesco
Schettino, Berlusconi akamgeukia mshambuliaji Balotelli na kusema:
'Nimekwisha. Sasa tupo na toto kutoka familia ya manyani. Ni kichaa.
Mabinti wote wanakaribishwa sana - unaweza pia kupata nafasi ya kuonana
na rais (Silvio Berlusconi).'
Balotelli alifunga mabao mawili katika mechi hiyo ya kwanza kuichezea AC Milan
Paolo
Berlusconi, ambaye pia ni Makamu wa rais wa AC Milan, pia ni Mhariri wa
gazeti la Giornale, ambalo kaka yake amekuwa akilitumia sana kwa mambo
yake ya kisiasa ya chama chake, People of Freedom na ndugu yake huyo
amekwishahusishwa na kashfa kibao za rushwa.
Balotelli kwa sasa yupo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Italia
No comments:
Post a Comment