Saturday, February 9, 2013

AUAWA MAITI YATUPWA NA KUTUPWA MTONI


                                    IGP Mwema

Na Anthony Mayunga-Mara.


WATU wawili wameuawa katika matukio mawili tofauti moja akidaiwa ni
wivu wa mapenzi katika wilaya ya Serengeti na mwingine boda boda
aliuawa na wananchi na maiti yake kutumbukizwa mtoni wilayani Butiama.

Matukio yote yamethibitishwa na Kamanda wa polisi mkoa wa Mara Absalom
mwakyoma yametokea kati ya februari 4 na 7 mwaka huu na kwa nyakati
tofauti.

Katika tukio la kwanza Mwita Wambura Wambura(28)mkazi wa kijiji cha
Nyamakendo kata ya Machochwe wilayani Serengeti anashikiliwa kwa
tuhuma za kumuua Rhobi Marwa Nyabange(32)mkazi wa kijijini hapo
kutokana na wivu wa mapenzi.

Kwa mjibu wa kamanda huyo tukio hilo limetokea februari 7 majira ya
saa 5 asubuhi mwaka huu kijijini hapo ambapo mtuhumiwa alimkata kwa
panga shingoni,shavu na mkono wa kushoto na kusababisha kifo chake.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa alikuwa na mahusiano na mama huyo ambaye
alikuwa mke wa mtu,na inasemekana Rhobi(marehemu)alisikitisha
mahusiano ghafla na mtuhumiwa uamzi ambao hakukubaliana nao na kuamua
kumuua wakati anakwenda kuchota maji kwenye lambo kijijini hapo.

Baada ya kutenda unyama huo wananchi walijitokeza akafanikiwa kukimbia
na kujisalimisha kituo kidogo cha polisi cha Machochwe kwa usalama
wake kwa kuhofu kuuawa na wananchi .

Katika tukio jingine Magera Mugeta(39)dreva boda boda mkazi wa Nyakato
Manispaa ya Musoma aliuawa na watu wasiojulikana na maiti yake
kutumbukizwa ndani ya Masimbi wenye kina cha urefu wa futi 3 ulioko
eneo la Nyegina.

Mwakyoma ameeleza kuwa maiti hiyo imeonekana februari 7 majira ya saa
4:00 asubuhi baada ya kuibuka na taarifa kutolewa polisi na kwa ndugu
zake.

Alisema februari 4 mwaka huu boda boda huyo katika eneo la Etaro kata
Etaro tarafa ya Makongoro wilaya ya Butiama alimgonga mtembea kwa
miguu aliyejulikana kwa jina moja la Majani na kuanguka akakimbia
akidhani ameua.

“Wananchi walimfukuza wakamkamata wakampiga na baada ya kumuua
wakamtumbukiza ndani ya mto hadi mwili wake ulipoibuka februari
7”alisema kamanda.

Na kuwa jeshi hilo linamshikilia Alex Nyarukamwa balozi wa nyumba kumi
katika eneo la Etaro aliyekutwa na pikipiki ya Marehemu yenye namba za
usajili P509 BCE ikiwa nyumbani kwake ikiwa ni baada ya siku tatu toka
mauaji hayo yametokea na hakuna sehemu aliyotoa taarifa.

Kufuatia taarifa hizo maboda boda kutokea Nyakato Manispaa ya Musoma
walikwenda kijijini hapo na kuchoma nyumba ya Koti Magere wakimtuhumu
kuhusika na mauaji hayo,upelelezi unaendelea ukikamilika watuhumiwa
wote watafikishwa mahakamani wakati wowote.


KWA MSAADA WA :http://francisgodwin.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment