WILAYA
YA CHUNYA – ASKARI POLISI MMOJA AUAWA KATIKA MAPAMBANO YA
KURUSHIANA RISASI NA MAJAMBAZI
ASKARI
Polisi mwenye namba G.68 PC Jafari Karume Mohamed (30), amefariki dunia
baada ya kurushiana risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi
wilayani Chunya mkoani Mbeya.
Taarifa ya kaimu kamanda wa polisi mkoani Mbeya Barakael Masaki
kwa waandishi wa habari iliyotumwa jana, ilisema kuwa kifo hicho
kimetokea leo Februari 6, mwaka huu katika hospitali ya wilaya ya
Chunya.
Alisema
kuwa chanzo cha tukio hilo ni majambazi waane wakiwa na silaha
idhaniwayo kuwa ya SMG walivamia kituo cha mafuta kilichopo kijiji cha
Matundasi mali ya Samora Muyombe na kupora fedha Sh. 2,200,000.
''Majambazi
hao walitumia gari T 227 BST aina ya Toyota Corola iliyokuwa
ikiendeshwa na Shaban Msule (33) mkazi wa Makambako mkoani Njombe''
alisema Kamanda Masaki.
Aliongeza
kuwa askari huyo aliyeuawa alikuwa doria na wenzake na walipofuatilia
tukio hilo na katika mapambano ya kurushiana risasi alijeruhiwa kwa
kupigwa risasi upande wa ubavu wa kulia na kukimbizwa hospitalini kwa
ajili ya matibabu zaidi.
Katika
mapambano hayo, jambazi Shaban Msule aliuawa kwa kupigwa risasi na gari
lililotumika katika tukio hilo limekamatwa na maganda 9 ya risasi aina
ya SMG/SAR na risasi 6 zimeokotwa eneo la tukio.
No comments:
Post a Comment