Hali ya utulivu inadaiwa kurejea katika wilaya ya Masasi mkoani
Mtwara baada ya vikosi vya jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) na
polisi kuungana kuweka ulinzi huku watu zaidi ya 40 wakikamatwa
kuhusika na matukio ya vurugu za jana.U
Mwandishi wa mtandao huu kutoka Mtwara John Kasembe anaripoti kuwa
kutokana na vurugu hizo waziri mkuu Mizengo Pinda na waziri wa mambo
ya ndani Dk Emmanuel Nchimbi usiku huu wapo Mtwara wakiendelea na
vikao vya kurejesha amani na utulivu mkoani hapo.
Pia inadaiwa mida ya asubuhi leo polisi walilazimika kutumia mabomu
ya machozi kuwatawanya vijana ambao walikuwa wamefunga barabara na
kuwatoza ushuru batili wa shilingi 5000 wenye magari kama sehemu ya
kujipatia fedha kwa njia feki.
Mbali ya tukio hilo bado katika mitaa mbali mbali ya Mtwara kwa siku
ya leo shughuli zote za uzalishaji mali zikiwemo biashara
zimesimamishwa kwa muda ili kukwepa vurugu kama za jana japo
shughuli za ibada zimeendelea kwa utulivu zaidi.
No comments:
Post a Comment