Mabingwa wa soka Tanzania bara Simba
wameanza vema michuano ya kombe la mapinduzi baada ya kufanikiwa kuifunga
Jamhuri ya Pemba kwa mabao 4-2 katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Amani Zanzibar.
Katika
mchezo huo ambao ulikuwa ni wa heshima ya uzinduzi wa michuano hii ya mwaka huu
2013 ambayo ni kuelekea katika sherehe za maadhimisho ya miaka 49 ya mapinduzi
ya Zanzibar ulianza kwa huku mvua ikinyesha na kufunguliwa na makamu wa kwanza
wa Rais Maalim Seif Sharif Hamadi.
Jamhuri
ndio walikuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za Simba kwa bao lililofingwa na
Mfanyeje Musa kabla ya Simba kusawazisha kupitia kwa Athumani Chanongo.
Jamhuri
kupitia tena kwa Mfanyeje Musa wakafanikiwa kuandika bao la pili kabla ya
Chanongo kusawazisha na timu hizo kwenda mapunziko zikiwa sare ya bao 2-2.
Kipindi
cha pili Simba ilifanikiwa kuandika mabao mawili yaliyofungwa na mzambia Felix
Sunzu na nahodha Shomari Kapombe.
No comments:
Post a Comment