Katibu wa mbunge bwana Antony Mlote akizungumza na viongozi wa kijiji cha Luponde wakati wa ziara yake katani humo.
Madarasa
katika shule ya msingi Luponde ambayo mabati yake yametolewa na mbunge
huyo na kisha kumuomba saruji kwa ajili ya ukamilishaji.
Hii ni
ofisi ya kijiji cha Miva ikiwa jirani kabisa na shule ya msingi ambayo
imetakiwa kujengwa upya kutokana na uchakavu wake.
Hapa anaelekea kukagua madarasa katika shule ya msingi Luponde ambapo mbunge huyo alitoa mabati takribani mia mbili.
Wakazi wa kijiji cha Lusitu wakimsikiliza katibu wa mbunge Anne Makinda akiwa amefika kusikiliza matatizo yao jana.
HUU Ni msingi wa ujenzi wa bweni la shule ya sekondari Luhololo katani humo likikaguliwa na katibu wa mbunge.
Baadhi
ya vijiji katika kata ya Luponde mkoani Njombe vimekosa mabati ya
ujenzi wa madarasa pamoja na nyumba za walimu yaliyokusudiwa kutolewa
kwa ahadi ya mbunge wa Jimbo la Njombe Kusini Anne Makinda kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu yao.
Miongoni
mwa vijiji vilivyokosa bati hizo takribani 100 ni pamoja na kijiji cha
Madobole ambacho hadi sasa kimeshindwa kujenga nyumba za walimu ambazo
mbunge huyo aliwataka waanze ujenzi wa nyumba hizo na kisha atoa bati
hizo.
Diwani wa kata ya Luponde bwana Romanus Mayemba amesema
kuwa kijiji hicho kimekosa bati hizo kutokana na matatizo ya uongozi wa
serikali ya kijiji hicho na si kwa matakwa ya wananchi.
Akihitimisha
ziara ya siku moja katika kata ya Luponde katibu wa mbunge wa Jimbo la
Njombe kusini bwana Antony Mlote Amesema kuwa pamoja na changamoto za
baadhi ya vijiji kukwama kutekeleza wajibu wao na kupelekea kukosa
misaada waliyotakiwa kuipata lakini kwa zaidi ya asilimia 90 vijiji
vimetekeleza na kutumia misaada waliyopewa
Aidha bwana Mlote
ameongeza kuwa kwa kawaida mbunge huyo hutoa baada ya wananchi kuanza na
hivyo kuitaka jamii kuendelea kubuni na kuibuwa vipaumbele vyao
vitakavyopelekea mbunge wao kuendelea kuwachangia katika shughuli zao.
Katika
hatua nyingine amesema kuwa ziara hiyo leo inaendelea katika kata za
Ihanga na na kisha atamalizia na tarafa ya Njombe Mjini kabla ya
kuelekea Mjini Dodoma kuwasilisha matatizo ya wananchi kwa mbunge
No comments:
Post a Comment