chanzo cha maji Ivalalila
Mmoja ya wafanyakazi ya maji wakipanda miti aina ya miturunga pembezoni mwa chanzo cha maji
Mamlaka ya maji katika mji wa Iwawa imeanza mikakati ya
kuboresha huduma hiyo ili kuondokana na shida ya upatikanaji wa maji kwa watumiaji
wa huduma hiyo.
Akizungumza na
kitulo fm meneja wa maji mjini hapa bwana Jornas Ndomba amesema kuwa tayari
wameshanza jitihada za kuongeza kingo za
pembeni katika chanzo kikuu cha mji kilichopo Ivalalila kwaajili kuzuia maji
mengi ili kutopungukiwa na maji hususani wakati wa kiangazi ambapo maji
hupungua na kutojitoshereza jambo ambalo lina leta kero kwawatumiaji wa huduma
hiyo.
Sambamba na hilo pia mamlaka ya maji
imepanda miti aina ya miturunga kuzunguka eneo la chanzo hicho cha maji kwa
ajili ya kuendelea kuongeza maji kwa wingi katika chanzo hicho .
Katika hatua
nyingine bwana Ndomba amewaomba wakazi wa Ivalalila kukitunza chanzo hicho kwa
kutoendeleza shughuli za kibinadamu katika chanzo hicho kwani kuna baadhi ya
watu wamekuwa na tabia ya kufanya shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo
ufungaji na upandaji wa miti bila kuzingatia sheria za ardhi jambo ambalo
linasababisha uhaba wa maji mjini hapa
No comments:
Post a Comment