MKUTANO wa wataalamu kati ya Tanzania na Malawi uliokuwa
ukifanyika jijini Dar es Salaam umeshindwa kupata suluhu ya mgogoro wa
mpaka wa Ziwa Nyasa.
Katika mkutano huo wa siku tatu ambao ulihitimishwa jana katika Hoteli ya Serena na mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi zote mbili, sasa wameamua kuupeleka mgogoro huo katika ngazi ya kimataifa.
Hayo yalielezwa jana wakati wakizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa pamoja uliofanywa na Mawaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe wa Tanzania na Mganda Chiume wa Malawi.
Mawaziri hao walisema kuwa kutokana na kushindwa kukubaliana huko wameamua kulipeleka suala hilo kwenye chombo kinachoundwa na Marais 10 wastaafu walichaguliwa kidemokrasia wanaojishughulisha na utatuzi wa migogoro chini ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
“Tunalichukua jambo hili, tunalipeleka kwa Marais wetu tumewapa miezi mitatu hadi Machi wazungumze wakikubali tutaandika barua ya pamoja na Machi 24 tutaipeleka katika chombo hiki, ” alisema Membe.
Alisema suala hilo litakapofikishwa katika chombo hicho cha SADC wamependekeza waalikwe na wataalamu wa kisheria wa ukanda wa Kusini mwa Afrika kwa ajili ya kusaidia utatuzi wa mgogoro huo.
Mawaziri wote wawili wamesema kuwa endapo chombo hicho kitashindwa kuleta suluhu, hayo yatakuwa ni mazungumzo ya mwisho na kwamba wataupeleka mgogoro huo katika Mahakama ya Haki ya Kimataifa ya ICJ.
Wakielezea kwa nini wameshindwa kufikia muafaka, Mawaziri hao walieleza mambo mawili ambayo wameshindwa kukubaliana nayo.
Kwanza ni Tanzania wameendelea kushikilia msimamo wao kwamba mpaka kati yake na Malawi ni katikati ya Ziwa Nyasa, huku Malawi wao wakishikilia msimamo wao kuwa Ziwa lote ni lao kwa upande wa Tanzania.
Pili, tofauti imejitokeza kwenye tafsiri ya kisheria kati ya Mwanasheria Mkuu wa serikali ya Tanzania, Frederick Werema na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri wa Sheria wa nchini Malawi, Ralph Kasambara.
Wanasheria hao Wakuu wa Serikali wametofautiana katika tafsiri ya Mkataba wa kuligawa Bara la Afrika ‘Heligoland Treaty’ hasa kwenye kifungu cha 1 (2) na kile cha 6.
Utata kuhusu ICJ
Kuhusu utata kwamba Tanzania si mwanachama wa ICJ, Membe alisema Tanzania ni mwanachama isipokuwa haitajaza azimio maalumu la ‘Comparison Declaration’.
Alisema kwa sababu Tanzania haijasaini azimio hilo, haiwezi kushitakiwa ila inaweza kumshitaki yeyote. Kwa upande wake Chiume wa Malawi, alisema wao ni wanachama wa ICJ na wamesaini azimio hilo.
Mawaziri wote wawili walisema kuwa, wanataka kuutatua mgogoro huu kwa njia ya kidiplomasia.
Waziri Chiume yeye alimshukuru Rais Kikwete kwa kuonesha nia hiyo na kumpongeza hotuba aliyoitoa Dodoma hivi karibuni wakati wa mkutano wa NEC akizungumzia kuhusu mgogoro huo.
Alisema Rais wao, Joyce Banda, anataka mgogoro huo usuluhishwe kwa njia ya amani.
Kuhusu mgogoro wa Ziwa Nyasa kujitokeza katika uongozi wa Banda, alisema jambo hilo limekuwa likihojiwa na watu wengi hata nchini Malawi.
Hata hivyo alisema kuwa jambo hilo lilikuwepo na hata Rais Bingu wa Mutharika aliliacha jambo hilo likiwa mezani.
Kadhalika mawaiziri wote wawili wamekataa kwamba mgogoro huo unatokana na rasilimali ya mafuta ambayo yamepatikana katika ziwa hilo.
Nyasa ni moja ya maziwa makubwa ya Afrika na ni la nane kwa ukubwa duniani.
Ziwa Nyasa linapakana na nchi za Msumbiji, Malawi na Tanzania.

No comments:
Post a Comment