Kutoka kushoto, Henry Kileo,
Nuru Ndosi
na Mhe. Godbless Lema wakiwa mahakamani leo.
Godbless
Lema akiwasili katika viwanja
vya Mahakama ya Kuu jijini Dar leo.
Pingamizi
lililowekwa na upande wa wajibu rufani
kupitia Wakili wao Alute Mughwai ili rufaa ya Lema kupinga kuvuliwa
ubunge
isisikilizwe limetupiliwa mbali na Mahakama baada ya kuridhika kwamba
kosoro
zilizolalamikiwa zilikuwa kwa upande wa Mahakama.
Pia kifungu kilichomhukumu Lema kina makosa hivyo kesi itatajwa tena baada ya siku 14 kwa ajili ya kuendelea kusikiliza hoja za waliokata rufaa. Mawakili wa Mhe. Godbless Lema wanahitajika kutimiza mahitaji fulani ya kisheria ndani ya siku 14 ili shauri la rufaa hiyo iweze kupangiwa siku ya kusikilizwa na kuamuliwa.
Wadaiwa kwenye shauri hilo ni wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo, waliofungua shauri lililotengua ubunge wa Lema wakidai kuwa wakati wa kampeni alimdhalilisha mgombea wa CCM, Dk. Batilda Burian kwa kutumia lugha za matusi. Lema anawakilishwa na Wakili Method Kimomogoro, anayesaidiana na Lissu.
No comments:
Post a Comment