Umoja wa waendesha pikipiki wilayani makete waamua kuunda chombo kitakachokuwa kikitetea haki zao baada ya kuibuka kwa wimbi la waendesha pikipiki wilayani hapa
Wakizungumza na mtandao huu madereva hao wamesema kuwa wamefikia harua hiyo baada ya kuona kuna dalili za ukiukwaji wa haki za madereva ha hasa miaka ya hivi karibuni baada ya kuibuka kwa wimbi la pikipiki nyingi maarufu kama bodaboda hivyo watu pamoja na serikali wamekuwa na mitazamo tofauti juu ya hivyo wamelazimika kufanya usajili huo
Pendekezo hilo wametoa hii leo kwenye mkuutano uliofanyika katika ukumbi wa halimashauri ya wilaya hii pia mkutano huo umeudhuliwa afisa biashara wa wilaya bwana Edonia Mahenge pia alikuwepo OCD akiwakilisha na Frenk Chimale kwa pamoja wametaka madereva hao kuongeza ushikiano huo pamoja na kufuata sheria za barabarani ikiwemo kuwa na Lesen ya udereva wa vyombo hivyo
Baada ya mkutano huo nilizungumza na baadhi ya madereva hao mmoja wao aliyejitambulisha kwa jina la Part amesema kuwa wameamua kufanya hivyo ilikuweka tashira nzuri kwa jamii ilikutoa imani ya kuwa wao ni wahuni jambo ambalo limekuwa likiwaghalimu na kuperekea kukosa soko kwa wateja wao
Ikumbukwe kuwa sehemu nyingi tanzania wamekuwa wakituma usafiri huo maarufu kama bodaboda na yeboyebo

No comments:
Post a Comment