Sunday, November 11, 2012

KANUMBA NA FREEMASONRY

  ULINGANO KATI YA KANUMBA NA WANJIRU


Kuna wengi ambao wameniandikia ujumbe mfupi wa maandishi katika simu pia katika facebook na wakikomenti kuhusu na uhalisia  wa Kanumba kuwa kipande cha Fraternal Organizational hapa ulimwenguni(Freemasons) huku wakipinga uwepo wake huko.

Ninachoweza kusema kwa sasa hebu twende taratibu utaelewa tu kwani sasa naomba nifungue Turbo zote kuhusu Freemasonry.
 ULINGANO KATI YA KANUMBA NA WANJIRU
Leo nataka nizungumzie  ulingano wa Steven Kanumba na Wanjiru
Wengi watakuwa wamesahau Wanjiru yule mwanariadha nguli wa Kenya ambaye alifariki Mei mwaka 2011.

MFANANISHO.
1.       Wote walikuwa ni vijana wa Ukanda wa Afrika Mashariki
2.      Wote walikuwa vijana waliofariki chini ya umri wa miaka 30; Wanjiru (24), Kanumba ( 28).
3.      Wote wamefariki kutokana na ugomvi wa kimapenzi. Kwani Wanjiru aligombana na mkewe wa ndoa Triza Njeri, Kanumba na mpenzi wake Elizabeth Michael(Lulu).
4.      Wote wamefia nyumbani kwa kudondoka. Wanjiru alidondoka kutoka balcony ya nyumbani kwake iliyopo Nyahururu kule Nakuru; Kanumba alidondoka nyumbani kwake Sinza Vatican Jijini Dar es Salaam.
5.      Wote katika vifo vyao KILEO kimetajwa.
6.      Wote kupitia vipaji vyao walijitahidi kujikwamua.

Sasa kwa leo nianze kwa salamu hizo kukuletea vitu vya kipekee kuhusu FREEMASONRY.

Kidogo kuhusu Samuel Kamau Wanjiru
Samuel Kamau Wanjiru (alizaliwa mnamo 10 Novemba, 1986 katika sehemu ya Nyahururu - 15 Mei, 2011) ni mwanariadha wa Kenya ambaye mbio zake maalum ni mbio za masafa marefu. Akawa mtaalamu katika umri mdogo na kuvunja rekodi ya dunia ya nusu marathon alipokuwa na umri wa miaka 18. Mwaka 2007, alivunja rekodi ya kukimbia ya barabara ya kilomita 20 na kuboresha rekodi ya nusu marathon kwa zaidi ya sekunde ishirini.

Alihamia hadi marathon kamili na alishinda katika Michezo ya Olimpiki ya Beijing ya mwaka wa 2008 kwa muda ambao ulikuwa rekodi ya Olimpiki wa masaa 2:06:32 na kuwa Mkenya wa kwanza kushinda medali ya dhahabu ya Olimpiki katika marathon. Mwaka uliofuata, alishinda marathon zote mbili za London Marathon na Chicago Marathon, kwa kukimbia marathon ya kasi zaidi milele kurekodiwa katika nchi za Uingereza na Marekani, mtawalia.

KWA MIEZI MITATU NITAKULETEA KILA SIKU KUHUSU FREEMASONRY.

No comments:

Post a Comment