Wednesday, November 7, 2012

JIMBO LA NJOMBE LASAIDIA UJENZI NYUMBA YA MWALIMU MAKETE




mwanahabari Edwini Moshi akizungumza na wanafunzi shuleni Makangalawe


Kanisa katoriki jimbo la Njombe limechangia zaidi ya shilingi milion kumi na sita kuajili  ujenzi wa nyumba ya  mwalimu katika shule ya msingi Makangalawe wilayani Makete.

    Akitoa taarifa mbele ya wandishi wa habari mwenyekiti wa kijiji hicho bwana Patrick Malumba asema ujenzi wa nyumba hiyo utaghalimu zaidi ya shilingi milioni ishirini huku wananchi wakichangia shilingi milioni nne na kanisa katoriki jimbo la Njombe likichangia shilingi milioni kumi na sita. 

    Bwana malumba amesema kuwa jengo hilo lilianza kujengwa  September mwaka huu linatajia kukamilika ifikapo desember 30 mwaka huu na kuanza kutumika mapema januari mwakani kwani shule hiyo  inakabiliwa  na uhaba wa nyumba za walimu kukamilika kwa jengo hilo kutasaidia kuongeza ufanisi kwa walimu na kuongezeka kwa ufaulu kwa wanafunzi katika mitiani ya kitaifa alisema Malumba.

    Mwisho bwana Malumba aliwashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kusaidia ujenzi huo pindi nguvu zao zinapohitajika  kwani mpaka sasa wapo hatua za mwisho za bimu na muda mfupi wataanza uezekaji wa jengo hilo.

No comments:

Post a Comment