Wednesday, November 21, 2012

CCM KUTOKA TINGATINGA HADI SHOKAMZOBA......





 Na mwanafasihi Mtanzania Profesa Kezilahabi anayesema haya: 


“ Siku hiyo ikifika utaona ishara itakayokuongoza. Utakapofika pale ambapo kila binadamu lazima afike utajua hukukosea; kwani njia ya kwenda huko inajulikana kwa wote na inakwenda moja kwa moja bila kupinda. Huna haja ya kusoma kitabu chochote kupata maelezo ya kwenda huko wala hakuna haja ya kusikiliza mahubiri. Hakuna utalaamu unaohitajika , maana utajikuta umefika. Utakapofika utamkuta amekaa peke yake akiwatazama wale wengine .

 Hao wengine utawatambua maana ni ndugu zako wote. Wengi kati yao ndio wale waliokuwa askari wa mwanga. Wale ambao hutaweza kuwatambua atakutambulisha kwao, na wewe utachukua nafasi yako. Usistuke utakaposikia majina yao; maana, wengi kati yao wana majina makubwa. Utawakuta wanafanya jambo fulani. Wewe pia fanya kama wao bila kuuliza , bila manung’uniko, na usikate tamaa. Kwa sasa hivi subiri ishara” ( E. Kezilahabi, Nagona) 

 Na kwa masikio yangu, nilipata kumsikia Philip Mangula akiyatamka haya mwaka 2007; “ Isifike mahali CCM ikatangaza tenda za uongozi!” Ilikuwa ni kwenye Ukumbi wa Mikutano wa St. Dominic, Iringa, Septemba 10, 2007. Ni kwenye Mkutano wa CCM Mkoa wa Iringa. Hiyo ilikuwa ni kauli nzito kutolewa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa zamani wa CCM. Mangula aliyatamka hayo wakati akitoa hotuba ya kushukuru wajumbe. Alishindwa nafasi ya Uenyekiti wa Mkoa, na aliambulia kura 332. 

Leo ndani ya CCM Mangula amepewa nafasi ya Umakamu wa Mwenyekiti wa CCM, Bara. Na majukumu makubwa mawili ya Makamu ni haya; Mosi, kumshauri Mwenyekiti, Pili, kusimamia maadili. Na tayari Mangula ametamka, kuwa ndani ya miezi sita atakuwa ameshakisafisha chama chake. Swali; Je, atawageukia pia ‘ waliomdhalilisha kisiasa’ pale Ukumbi wa St. Dominic Iringa mwaka 2007? Naliona tatizo linaloikabili CCM kama Chama cha siasa.... Soma zaidi: http://www.kwanzajamii.com

No comments:

Post a Comment