Sunday, October 28, 2012

CHICHARITO ABOMOA DARAJA STAMFORD!


>>CHELSEA wamaliza Mechi Mtu 9!!
MAN_UNITED_WALL++++++++++++++++++++++
MATOKEO:
Jumapili, Oktoba 28
Everton 2 Liverpool 2
Newcastle United 2 West Bromwich Albion 1
Southampton 1 Tottenham Hotspur 2
Chelsea 2 Manchester United 3
++++++++++++++++++++++
Manchester United waliwazidi nguvu Mtu 9 Chelsea na kuwatwanga bao 3-2 katika Mechi kali ya Ligi Kuu England iliyochezwa leo Uwanjani Stamford Bridge na kuwafanya Man United waikaribie Chelsea kileleni na kuwa Pointi 1 tu nyuma yao lakini Refa Mark Clattenburg aliibua maswali mengi baada ya kuwatwanga Wachezaji wawili wa Chelsea Kadi Nyekundu
Man United waliingia Uwanjani kwa mori na kupiga ba0 2-0 kupitia bao la kujifunga mwenyewe David Luiz baada ya shuti la Robin van Persie kupiga posti na kumbabatiza Luis na kutinga kisha likafuata bao la Robin van Persie kufuatia muvu nzuri sana ya Man United.
+++++++++++++++++++++++
MAGOLI:
Chelsea:
-Mata, Dakika ya 44
-Ramires, 53
Man United:
-David Luiz, Dakika ya 4 [Kujifunga mwenyewe]
-Robin van Persie, 12
-Chicharito, 75
+++++++++++++++++++++++
Lakini frikiki tamu ya Juan Mata na kichwa cha Ramires lakaifanya Mechi iwe 2-2 a ndipo balaa likashuka kwa Chelsea.
Branislav Ivanovic akatolewa nje kwa Kadi Nyekundu kwa kumchezea rafu Ashley Young akiwa Mtu wa mwisho na Fernando Torres kwa kujiangusha.
Lakini, marudio ya Video yalionyesha Fernando Torres hakujiungusha bali aliguswa na Jonny Evans.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO Timu za juu:
[Kila Timu imecheza Mechi 9]
1 Chelsea Pointi 22
2 Man United 21 [Tofauti ya Magoli 11]
3 Man City 21 [Tofauti ya Magoli 9]
4 Tottenham 17
5 Everton 16
6 Arsenal 15
7 Fulham 14
8 WBA 14
9 West Ham 14
10 Newcastle 13
+++++++++++++++++++++++
Hata hivyo, Javier Hernandez, alieanzia benchi, aliipigia Man United bao la 3 na kuipa ushindi.
VIKOSI:
Chelsea: Cech, Ivanovic, Luiz, Cahill, Cole, Mikel, Ramires, Hazard, Oscar, Mata, Torres
Akiba: Turnbull, Romeu, Moses, Marin, Sturridge, Azpilicueta, Bertrand.
Man United: De Gea, Da Silva, Ferdinand, Evans, Evra, Valencia, Carrick, Cleverley, Young, Rooney, van Persie
Akiba: Lindegaard, Anderson, Giggs, Hernandez, Nani, Welbeck, Scholes.
Refa: Mark Clattenburg
Newcastle 2 West Brom 1
Bao la Dakika ya 90 baada ya shuti la Sammy Ameobi kumbabatiza Papiss Cisse limewapa ushindi Newcastle wakiwa kwao St James Park kwa kuichapa WBA bao 2-1 Uwanjani St James Park.
Newcastle walitangulia kufunga kupitia Demba Ba na Romelu Lukaku kuisawazishia WBA.
VIKOSI:
Newcastle: Krul, Simpson, Coloccini, Williamson, Santon, Ben Arfa, Cabaye, Perch, Gutierrez, Ba, Shola Ameobi. Subs: Harper, Anita, Cisse, Obertan, Steven Taylor, Sammy Ameobi, Ferguson.
West Brom: Foster, Tamas, McAuley, Olsson, Ridgewell, Morrison, Gera, Mulumbu, Dorrans, Odemwingie, Lukaku. Subs: Luke Daniels, Popov, Rosenberg, Long, El Ghanassy, Jara Reyes, Fortune.
Refa: Chris Foy
Southampton 1 Tottenham 2
Tottenham Hotspur wamechupa hadi nafasi ya 4 baada ya kuichapa Southampton 2-1 kwa bao za Gareth Bale na Clint Dempsey lakini Southampton wakafunga bao lao kupitia Jay Rodriguez na kuifanya imalizike ikiwa mshikemshike.
VIKOSI:
Southampton: Boruc, Clyne, Yoshida, Fonte, Fox, Puncheon, Schneiderlin, Steven Davis, Lallana, Lambert, Rodriguez. Subs: Kelvin Davis, Hooiveld, Ward-Prowse, Do Prado, Mayuka, Chaplow, Reeves.
Tottenham: Friedel, Walker, Caulker, Gallas, Vertonghen, Sandro, Huddlestone, Lennon, Dempsey, Bale, Defoe. Subs: Lloris, Naughton, Dawson, Sigurdsson, Falque, Livermore, Townsend.
Refa: Lee Mason
RATIBA MECHI ZIJAZO LIGI KUU ENGLAND:
Jumamosi, Novemba 3, 2012
[SAA 8 Dak 45 Mchana]
Manchester United v Arsenal
[SAA 12 Jioni]
Fulham v Everton
Norwich City v Stoke City
Sunderland v Aston Villa
Swansea City v Chelsea
Tottenham Hotspur v Wigan Athletic
[SAA 2 na Nusu Usiku]
West Ham United v Manchester City
Jumapili, Novemba 4, 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Queens Park Rangers v Reading
[SAA 1 Usiku]
Liverpool v Newcastle United
Jumatatu, Novemba 5, 2012
[SAA 5 Usiku]

No comments:

Post a Comment