Tuesday, October 2, 2012

chadema wajikanyaga makete



Katika hali ambayo haikutegemewa na wengi, katibu wa itikadi na uenezi wa CHADEMA wilayani Makete Bw. Sinene amekifagilia chama cha mapinduzi kwa kusema kuwa kimejitahidi katika mambo yake ikiwemo kuwa na wanachama wengi wilayani hapo kwa zaidi ya asilimia 90 

Sinene ameyasema hayo alipokuwa akitoa nasaha zake alipoalikwa kuhudhuria mkutano wa uchaguzi wa CCM uliofanyika jana kwenye ukumbi wa shule ya sekondari Iwawa wilayani hapo
Katibu huyo alisema “nikilinganisha huko nyuma na hii leo kwa kweli chama chenu kimejitahidi kwa zaidi ya asilimia 90, mna wanachama wengi na mnaendelea kufanya mengi”
Awali wakati akianza kutoa salamu zake alisema unapokwenda sehemu inabidi utumie taratibu za eneo hilo, hivyo kulazimika kusema ‘CCM hoyeeeeeee’ hali iliyowafurahisha wajumbe wa mkutano huo wakiwemo viongozi wa CCM
Baada ya kumaliza salamu zake hizo kulipelekea utani wa hapa na pale ikiwemo kumvalisha kofia ya CCM ingawa alikataa kuivaa huku wengine wakitaka kumpa shati la kijani, na sauti za kumkaribisha CCM zikisikika
Akizungumza mara baada ya kiongozi huyo wa CHADEMA kumaliza kutoa salamu zake, katibu wa CCm wilaya ya Makete Miraji Mtaturu alisema ni kweli chama chake ni kikubwa na wapinzani watazidi kupata tabu kama alivyokiri mwenyewe
“Ndugu wajumbe kauli ya katibu mwenezi wa CHADEMA mmeisikia wenyewe, kwa kawaida katibu mwenezi ni msemaji wa chama, hivyo kauli yake ni kauli ya chama, nachopenda kumwambia hakuna haja ya kupoteza muda, njoo CCM ndugu yangu” alidai Mtaturu
Kauli hiyo ya katibu mwenezi wa CHADEMA ilizua gumzo
 miongoni mwa wanachama wake waliokuwa nje ya ukumbi huo huku wakisikika wakisema amejimaliza kisiasa na kuona hana haja ya kuendelea kuwepo ndani ya Chadema na badala yake ahamie CCM aliyoifagilia
Kauli hiyo pia ilitumiwa na wagombea wa CCM katika uchaguzi huo hasa wale waliokuwa wakitetea nafasi zao akiwemo Mzee Mwamwala kwa kusema kuwa “katika uongozi wangu nimefanya mengi mazuri hadi mmesikia mwenyewe CHADEMA wanaikubali CCM na wasingeikubali bila uongozi wangu mahiri, hivyo naomba kura zenu”
Pamoja na kutumia fursa hiyo Mzee Mwamwala alishindwa kutetea kiti chake na nafasi yake ilichukuliwa na Francis Chaula aliyepata kura 791 dhidi ya Mwamwala aliyepata kura 155

2 comments:

  1. Mind your heading spelling(chadema wajikanyaka makete)KUJIKANYAKA

    ReplyDelete