Saturday, August 25, 2012

SENSA YA WATU NA MAKAZI KUANZA LEO SAA 6 USIKU


SENSA YA WATU NA MAKAZI KUANZA LEO SAA 6 USIKU ITADUMU SIKU SABA JIANDAE KUHESABIWA



Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr.Christine Ishengoma amewataka wananchi wa mkoa wa Iringa kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa ya watu na makazi ,zoezi litakaloanza usiku wa leo jumamosi ya Agost 25 kuamkia Agost 26 mwaka huu.

Mkuu huyo wa mkoa ameyasema hayo wakati wa mahojiano maalum na mtandao huu wa www.francis Godwin.blogspot.com kuhusiana na maandalizi ya zoezi hilo kwa mkoa wa Iringa.

Amesema kuwa hadi sasa mandalizi ya zoezi la sensa kwa mkoa wa Iringa yamefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 90 na kuwa wananchi wote wanapaswa kutoa ushirikiano wao kwa makarani wa sensa watakaofika katika maeneo yao.

Dr.Ishengoma amesema kuwa zoezi hilo la Sensa ni kwa watanzania wote hivyo lazima makundi yote kujitokeza kuhesabiwa bila kuwabagua wazee,walemavu katika kuhesabiwa .

Ametaka wakuu wa kaya kutoa ushirikiano wa kutosha kwa makarani wa Sensa na kuwa mkuu wa kaya atakayewazuia makarani wa sensa kuifanya kazi hiyo hatua kali atachukuliwa .

1 comment: