NA
RIZIKI MANFRED
BONZUMA
5/6/2012
MAKETE
Chama cha mapinduzi wilayani
makete kimepongeza tamko la Rais kuhusu mgomo wa madaktari alilolitoa
kupitia hotuba yake ya mwishoni mwa mwezi jun mwaka huu
akizungumza na kwanza jamii kwaniaba ya chama cha mapinduzi katibu
wilaya ya makete bwa Mlaji mtaturu amesema kuwa anapongeza hatua aliyo
ichukua rais wa jamhuri ya muungano waTanzania mheshimiwa Jakaya Mlisho
Kikwete kwakuwataka madaktari kurudi kazini haraka iwezekanavyo kwani
kufanya hivyo kumenusuru maisha ya wengi kwani mgomo huo ulikuwa
ukiwalenga zaidi wananchi wa hali ya chini hivyo kwa tamko la Rais
amewakomboa watanzania
Aidha bwana Mtaturu
ametumia muda huo kuwapongeza madaktari wa wilaya Makete kwa kutoshiriki
katika mgomo huo licha ya madaktari wasehemu zingine kuendea
kushinikiza mgomo huo karibu nchi nzima lakini hali ilikuwa
tofauti''nawashukuru madkitari wa makete kwakutojiingiza katika mgomo
huu na kundelea kuwahudumia wagonjwa jambo ambalo linaijengea heshima
wilaya Makete ''alisema Mtaturu na kuongeza kuwa jambo la kuigwa kwa
madaktari wengine nchini kwani kwa kufanya hivyo unalijengea heshima
taifa la Tanzania
akiendelea bwana
Mtaturu ameungana na watanzania wengine kutoa pole kwa dk Ulimboka kwa
kitendo alichofanyiwa ambacho amekiita sio cha kiugwana na kukemea tabia
hiyo nakuomba hatua kali zichukuliwe kwa wahusika
No comments:
Post a Comment