Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard
Membe, ametangaza rasmi nia ya kuutaka urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania 2015 akisema anatosha na kwamba Baba wa Taifa, Mwalimu Julius
Nyerere huko aliko atafurahi endapo atakuwa rais.
Membe aliyasema hayo jana kwenye Viwanja vya Ofisi
ya CCM Mkoa wa Lindi katika hotuba yake ya saa moja kutangaza nia yake
hiyo huku kwa kujiamini kabisa akisema kuwa yeye ndiye Rais wa Tanzania
kwa miaka 10 ijayo.
Alisema katika urais wake, ataboresha elimu,
ataweka msisitizo katika utawala bora, maendeleo ya jamii, uchumi na
masuala mbalimbali ya kisiasa na kidiplomasia.
Huku akishangiliwa na maelfu ya watu waliofika kumsikiliza, alisema amejipima na kuona anaweza.
“Nimetafakari sana, nimeona ninatosha kwa nafasi
hii nyeti…, nafasi adhimu na si ya mzaha japo naona wapo wanaofanya
mzaha. Nimeangalia nikaona hakuna mwingine wa kufanana na mimi.
“Sikukurupuka, zipo nafasi za kukurupuka na wapo wanaokurupuka, lakini si vyema kukurupuka kwa nafasi ya urais,” alisema.
Membe aliyesindikizwa na mkewe Dorcas, alisema
Machi mwaka huu alikwenda Butiama na kuzuru kaburi la Mwalimu na kupiga
goti na kumweleza nia yake ya kuutaka urais.
“Nilipiga goti nikamwambia Mwalimu, navitaka viatu
vyako, alivivaa Mzee Mwinyi (Ali Hassan), Mzee Mkapa (Benjamin) na
Kikwete (Jakaya), sasa nataka kuvaa mimi na nina hakika vinanitosha.
“Ninaamini vitanitosha. Nikamwambia chondechonde,
kama havitanitosha, niambie… timu yangu ya mikoani ikawahi kuniambia
unatosha,” alisema Membe.
Alisema alialikwa na Mzee Mwinyi katika ‘birthday’
yake ya miaka 91 na kati ya mambo aliyomwambia ni kwamba ameongoza
nafasi mbalimbali, lakini hakuwahi kununua uongozi.
“Mzee Mwinyi aliniambia kuwa alipata vyeo bila
kununua, alisema sikuwa na magunia ya pesa miee…, sikununua wajumbe.
Sasa, utajisikiaje kununua vyeo? Utawaangalia kwa jicho gani wanapokosea
na utachukua hatua gani kuwawajibisha? Kuna vitu vya kununua lakini si
Ikulu. Ikulu hainunuliki.”
Utawala bora
No comments:
Post a Comment