Habari kutoka mkoani Ruvuma zinasema
kuwa wanafunzi 16 wa shule ya sekondari ya Misheni ya Kigonsela wilaya
ya Mbinga wanadaiwa kupoteza maisha na wengine 24 kujeruhiwa vibaya
katika gari linalomilikiwa na mwalimu mkuu wa shule hiyo.
Ajali hiyo imetokea katika eneo la kijiji cha Kigonsela kata ya Kigonsela baada ya gari dogo aina ya Landrover 110
lenye milango mitano kushindwa kupanda mlima na kupinduka kwenye korongo kisha kuwaka moto.
Wanafunzi hao walikuwa wanatoka kwenye shamba la shule kurudi shule,walifuatwa na mkuu wa shule hiyo.
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari
Ngaiwona Nkondola aliyeongea na kamanda wa polisi mkoani humo,huenda
ajali hiyo imetokana na kuzidiwa kwani ndani ya gari hilo kulikuwa na
wanafunzi 16 ambao wote wameteketea kwa moto pamoja na mwalimu wao huku
juu ya gari (keria) wakiwa wamekaa wanafunzi zaidi ya 20 ambao
wamejeruhiwa vibaya.
KWA HISANI YA MALUNDE BLOG
No comments:
Post a Comment