Wizara ya Sheria ya Marekani
imechapisha taarifa inayoelezea jinsi Afisa wa zamani wa FIFA Chuck
Blazer alivyokiri kuwa yeye pamoja na wenzake walipokea rushwa ikiwa ni
pamoja kuichagua Afrika Kusini kuwa mwenyeji wa fainali ya kombe la
dunia mwaka 2010.
Katika taarifa hiyo imeweka wazi mtandao wa
malipo ya rushwa ulivyokuwa ukifanywa ndani ya shirikisho la soka
duniani FIFA, taarifa zinazoegemea uchunguzi uliofanywa na shirika la
kijasusi la Marekani FBI.
Taarifa hiyo ambayo inamwelezea Afisa
humo wa zamani wa Fifa Chuck Blazer kukiri kupokea rushwa sasa huenda
ikaibua mengi kwenye kashfa ya rushwa inayoindamana shirikisho la FIFA.
Mmerakani
huyo kwenye taarifa hiyo inadai alikuwa ni mmoja wa watu waliosuka
mipango ya kupokea rushwa katika tukio jingine la fainali la kombe la
dunia 1998.
Taarifa za Kukiri zipo katika maandishi wakati wa kesi
yake mwaka 2013 wakati kesi yake ilipokuwa akisikilizwa katika mahakama
ya Easten New York huko Marekani ambapo alikiri makosa kumi yaliyokuwa
yanamkabili.
Blazer alikuwa afisa wa ngazi juu wa FIFA eneo la
kanda ya Amerika Kaskazini na Kati na ukanda wa nchi Caribbean kuanzia
mwaka 1990 hadi mwaka 2011.
Marekani imefungua kesi ya rushwa
inayowakabili maafisa wa FIFA jambo lililofanya Rais wa FIFA Sepp
Blatter kuamua kutangaza kujiuzulu.
Mwendesha mashtaka wa Marekani
wiki iliyopita aliwashtaki maafisa 14 wa ngazi wa juu wa FIFA tuhuma za
rushwa, kutakatisha fesha,
No comments:
Post a Comment