Thursday, November 28, 2013

PUA BANDIA YAGUNDULIWA HUKO SINGAPORE

MAJUU BWANA
*Mtu hunusa ladha ya chakula akitazama picha
SINGAPORE CITY, Singapore

KADIRI siku zinavyokwenda ndivyo wanasayansi wanavyogundua vitu mbalimbali ambapo wametengeneza kifaa ambacho kinaweza kuufanya pua inuse harufu ya chakula kwenye picha kwenye kompyuta.
Kifaa hicho kinaweza kumfanya mtumiaji wa kompyuta hususan anayefungua mtandao wenye picha za vyakula pindi aangaliapo anaweza kunusa harufu yake.
Kama mtu ataangalia kupitia mtandao juisi, keki au nyama zilizorostiwa ulimi wake utatokwa na mate kutokana na hamu ya kula.
Jopo la wanasayansi wa chuo kikuu kimoja nchini Singapore wametengeneza kifaa hicho ambacho kipo katika mfumo wa digitali.
Mtafiti Mkuu wa jopo hilo, Nimesha Ranasinghe alisema kama binadamu ana aina za fahamu ambazo ni kuona kwa kutumia macho, kugusa (ngozi), kusikia (masikio) na pua ambayo wameiboresha.

No comments:

Post a Comment