Tuesday, November 26, 2013

JAMBAZI AJITWANGA RISASI KWA HOFU YA KUDAKWA

MTU mmoja anayedaiwa kuwa jambazi amejikuta akijitwanga risasi mwenyewe kutokana na wasiwasi wa kutiwa mbaroni baada ya kupora benki.
Njemba huyo akiwa na wenzake waliingia katika benki hiyo na kupora dola takriban 16,000 lakini kutokana na wasiwasi huo alijipiga risasi.
Kwa mujibu wa picha za video za usalama (CCTV) zilizopo katika benki hiyo watu watatu wakiwa na silaha waliingia na kufanya uhalifu huo.
Baada ya kufanikiwa kupora minoti hiyo hata hivyo mmoja wao aliyekuwa mlangoni alionekana akiwa na hali ya wasiwasi muda wote wakati wizi unaendelea.
Akiwa ameshika bastola mbili alionekana kutokuwa na hali ya utulivu na ghafla alijitwanga risasi mwenyewe mguuni.
Hata hivyo waswahili wanasema mbio za panya huishia sakafuni siku iliyofuata alikamatwa baada ya kwenda hospitali kutafuta matibabu ya mguu wake

No comments:

Post a Comment