BUKOBA, Tanzania
Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kimeamua kuwatolea uvivu kwa kuwavua uanachama na
uongozi madiwani wake wanane katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
mkoani Kagera.
Imeelezwa
kwamba hatua hiyo imechukuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Kagera
kutokana na kudaiwa kupuuza maelekezo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa CCM,
Taifa, Rais Jakaya Kikwete.
Taarifa
iliyotolewa na Katibu wa CCM wa mkoa huo Avelin Mushi, na theNkoromo
Blog kuipata, imesema kuwa uamuzi huo umekuja kutokana na chama kujali
maslahi ya wananchi tofauti ya watu binafsi.
Mushi amewataja
madiwani hao nane kuwa Yusuph Ngaiza (Kata Kashai) ambaye pia ni
Mwenyekiti wa CCM wilaya Bukoba, Samwel Ruangisa (Kitendagulo) ambaye ni
Meya mstaafu na Mkuu wa mkoa wa mkoa wa kwanza wa mkoa wa Kagera,
Murungi Kichwabuta (Viti maalumu) Deusdedith Mutakyawa (Nyanga) Richard
Gaspal (Miembeni)Alexander Ngalinda (Buhembe) ambaye pia alikuwa Naibu
MeyaDauda Kalumuna (Ijuganyondo) na Robert Katunzi wa kata Hamugembe.
Mushi amesema
kuwa kufukuzwa kwa madiwani hao ni kutokana na mgogoro ulidumu kwa muda
mrefu juu ya mbunge na meya ambapo Rais Kikwete akiwa ziarani Kagera
alitoa agizo la wanachama hao kutoendelea na mgogoro huo.
Pia, amesema
kuwa vikao vya chama vimekuwa vikiendelea kwa kufuata kanuni na taratibu
kwa kuwaonya juu ya kuhujumu serikali ya CCM kwa kushirikiana na
madiwani kambi ya upinzani kutotekeleza maendeleo ya wananchi lakini
wahusika wote wamekuwa wakikahidi maagizo ya kuitwa kwenye vikao.
No comments:
Post a Comment