Monday, July 22, 2013

M 23 WAJIGAMBA KUMSHIKILIA ASKARI MTANZANIA

KUNDI la Waasi wa M23 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), limedai kumkamata askari anayedaiwa kuwa ni wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), aliyetambulika kwa jina la Christopher George Yohana. Askari huyo inasemekana alikamatwa wakati alipokuwa akishirikiana na waasi wa Rwanda (FDLR), wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya maelfu ya Watutsi mwaka 1994.

Tukio hilo limekuja siku moja baada ya kuwasili kwa miili ya askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), waliouawa na kundi la waasi katika Jimbo la Darfur nchini Sudan.

Askari hao, waliuawa wakati walipokuwa wanasindikiza msafara wa maofisa wa Umoja wa Mataifa nchini humo.

Taarifa zilizopatikana kupitia mtandao wa Chimpreports.com (CR) wa nchini Uganda na baadaye taarifa zake kusambazwa katika mitandao mingine ya kijamii, waasi wa M23 walimkamata askari huyo akiwa na bunduki aina ya AK47 yenye namba 1372.

No comments:

Post a Comment