Dodoma. Polisi mkoani hapa wamewataka wananchi kujiepusha na
matapeli ambao wamejitokeza kwa wingi kwa siku za hivi karibuni na
kuwatapeli watu wengi.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, David Misime alitoa
wito huo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake
kufuatia kuibuka kwa wimbi la matapeli mjini hapa.
Alitoa kauli hiyo kufuatia kuwapo kwa matapeli
ambao walichukua fedha za watu wengi wakidai watatoa ajira kwa kazi ya
kuandikisha watu wanaotaka vitambulisho vya taifa.
Misime alisema watu wanapaswa kupata taarifa sahihi.
No comments:
Post a Comment