katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Taifa Nape Nnauye akisalimiana na wananchi wa wilaya ya Ludewa
Katibu mkuu wa CCM Taifa Bw.Kinana akisalimiana na Baba mzazi wa Mbunge wa jimbo la Ludewa Mzee Filikunjombe
Kinana akiongea na wananchi wa kata ya Ludewa mjini
Wananchi wakimsikiliza mbunge wao Deo Filikunjombe hayupo pichani
Wananchi wakifuatilia mkutano wa hadhara
Katibu mkuu wa chama cha
mapinduzi Taifa Bw.Abdulrahman Kinana jana aliwahakikishia wananchi
wa wilaya ya Ludewa katika Mkoa wa Njombe kuwa viwanda vya uzalishaji wa chuma
na makaa yamawe vitajengwa wilayani humo na si
kwingineko.
Kauli hiyo ya Kinana
imekuja baada ya kuvuma tetesi kuwa viwanda hivyo kunauwezekano mkubwa wa
kujengwa Bagamoyo hivyo wananchi wa wilaya ya Ludewa walikuwa na shauku ya kujua
ujemzi wa viwanda hivyo.
Alisema kutokana na ukubwa
wa miradi hiyo miwili ambayo inatarajia kuanza miaka ya 2015 na 2016 na kubadiri
taswira nzima ya wilaya ya Ludewa haitaweza kujengwa eneo jingine zaizi ya
wilaya hiyo na kusambaza umeme huo nchi nzima.
Bw. Kinana aliwataka
wananchi wa wilaya hiyo kuwa makini na watu wanaoeneza habari za uwongo ambazo
zinalengo la kujenga chuki miongoni mwa jamii na viongozi kwani kinachotakiwa
zaidi ni kuisikiliza Serikali kupitia kwa Mbunge wa jimbo
hilo.
“Tumekuwa tukifanya kazi
vizuri na Mbunge wenu Filikunjombe hivyo kinachotakiwa kumsikiliza na kumuamini
kwani chochote anachowaeleza kinatoka Serikalini na si vinginevyo hata hao
wanowadanganya kuhusiana na ujenzi wa viwanda wakataeni”,alisema
Bw.Kinana.
Alisema Serikali ya CCM
inafurahishwa na utendaji wa Mh.Deo Filikunjombe kwani ni mfano kwa wabunge
wengine wa chama hicho kutokana na kujiamini katika kutetea wananchi wake awapo
Bungeni.
Katika hatua nyingine Wananchi
wa jimbo hilo walionyesha kumbana kiongozi huyo kwa kuhoji sababu ya
wabunge wa CCM bungeni kufanya kazi ya kukipongeza chama chao huku wengi
wao wakiwa kimya (mabubu) katika kuchangia na wale wanaochangia kama mbunge
wao Filikunjombe wamekuwa waklichukiwa kuwa ni wapinzani ndani ya CCM
.
Hivyo wananchi hao kumweleza
katibu mkuu huyo aliyeongozana na katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Taifa
Nape Nnauye kuwa wao wataendelea kumuunga mkono mbunge Filikunjombe kwa
vipindi vingine tena vitatu vya miaka 15 hadi mbunge mwenyewe atakapoamua
kuacha kugombea na iwapo watafanya mchezo basi wao watamfuata mbunge huyo
kokote atakakokuwa.
" Mheshimiwa tunaomba leo
chama kitueleze hivi kwanini wabunge wa CCM wamekuwa si msaada kwa wapiga
kura wao muda wote wamekuwa kimya bungeni na wale wanaochangia
wanachangia kupongeza chama, tunaomba kukueleza kuwa sisi tupo na mbunge
wetu na hata wana CCM wanaojipitisha jimbo la Ludewa wakiamini sisi
tutayumba uwaeleze kuwa CCM hatudanganyiki "alihoji mwananchi aliyejulikana
kwa jina la Optatus Kalungu.
Akizungumza jana na wananchi
wa wilaya ya Ludewa ambao walikusanyika kwa wingi katika mkutano wa hadhara
kwa lengo la kutaka kusikia kauli ya CCM juu ya uamuzi utakaochukuliwa kwa
mbunge wao kutokana na kuwepo kwa kauli za chini kwa chini katika jimbo hilo
kuwa ziara ya Kinana jimboni humo ni kutaka kumshughulikia mbunge
huyo.
Hata hivyo Kinana aliwataka
wananchi wanaounga mkono uamuzi wa kuendelea kumwongezea muda wa vipindi
vitatu Filikunjombe kunyosha mikono juu na baada ya wananchi wote
kunyosha mikono yao juu alisema pia kwa upande wake anaungana na wao na kuwa
chama hakitafanya makosa kwa kuwasaliti kuwapa mtu mwingine katika uchaguzi
ujao wa mwaka 2015 .
"Hata mimi katibu mkuu
naungana na uamuzi wenu wa kumwongeza muda Filikunjombe na napenda
kuwahakikishia kuwa CCM haitafanya makosa itaendelea kuwaachia Filikunjombe
kama mlivyomchagua wenyewe labda ashindwe yeye " alisema
Kinana.
Kwa upande wake Filikunjombe
alisema mbali ya kuanza mradi mkubwa wa lami katika wilaya hiyo wa kuanzani
Itoni Njombe hadi Manda ila bado kuna mradi wa maji wenye thamani ya Tsh
bilioni 1.5 ambao utaondoa adha ya maji katika mji wa Ludewa ambayo ndio kero
kubwa kwa wananchi wake.
Filikunjombe alisema katika
mji wa Ludewa tayari Serikali imetenga fedha za kutengeneza barabara za mitaa
kwa kiwango cha lami kilometa kumi na ujenzi huo unaanza mara moja hivi punde
hivyo wananchi wanatakiwa kutoa ushirikiano kwa kampuni iliyopewa tanda
hiyo.
Alisema kutokana na kuendelea
kuutamani ubunge wake ataendelea kuwatumikia vema wananchi na kamwe siku
zote hatarudi nyuma bungeni katika kuwapigania wananchi hao
No comments:
Post a Comment