Na Edwin Moshi, Makete
Vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vinavyoendelea kufanyika
kwa wanafunzi wa shule za sekondari wilayani makete mkoani Njombe ni miongoni
mwa visababishi vikubwa vinavyochangia wanafunzi kutofikia malengo yao
Hayo yamebainika wakati wanafunzi wa shule ya sekondari Mlondwe
ilkiyopo kata ya Itundu wilayani hapo wakizungumza na mtandao huu wakati wa
kuandaa vipindi vya redio shuleni hapo kwa ushirikiano na shirika la SUMASESU,
ulipotaka kufahamu sababu zinazopelekea wanafunzi kushuka kitaaluma siku hadi
siku katika shule za sekondari wilayani Makete
Mmoja wa mwnafunzi aliyejitambulisha kwa jina moja la Sanga ambaye
anasoma kidato cha tatu shuleni hapo amevitaja baadhi ya vitendo vya
unyanyasaji wa kijinsia wanavyofanyiwa wanafunzi wawapo shuleni kuwa ni
wanafunzi wa kidato cha kwanza kutishiwa, wavulana kunyang’anywa sahani zao
wakati wa kula na wanafunzi wa vidato vya juu kwa madai kuwa wao ni watoto wa
kiume wanaweza kuvumilia njaa pamoja na vipigo vya mara kwa mara
“Unakuta mwanafunzi anakuita wewe wa form one (kidato cha
kwanza) anakunyang’anya sahani yako na ukileta ubishi anaitumia halafua
anaipasua, unakuta mimi sina nguvu za kumpiga na pia naogopa kwenda kusema kwa
mwalimu sasa hii kwa kweli sidhani kama mwanafunzi ataitamani shule, nia lazima
afeli”alisema Sanga
Kwa upande wake Emmy anayesoma kidato cha pili shuleni hapo
amesema wapo baadhi ya wanafunzi wa kiume ambao wanakaguliwa na wavulana wa
vidato vya juu kama wamedondosha mkono sweta (wamefanyiwa tohara) na endapo
itagundulika hawajatahiriwa huambulia kipigo na vitisho, adhabu kutolewa bila
usawa na wakati mwingine adhabu kali zaidi, pamoja na wanafunzi kujihusisha
kimapenzi na waalimu na wanafunzi wenzao
Awali mratibu wa program ya shule salama kutoka shirika la
SUMASESU Bi Anifa Mwakitalima aliwataka wanafunzi hao kutokuwa na woga wa
kuvitaja vitendo hivyo wanavyofanyiwa kwa madai ya kuogopa ama kuona kama ni
vitendo vya kawaida, na badala yake waseme ukweli ili vitendo hivyo vikomeshwe
“Unaweza kukuta wakati vipindi hivyo vitakapoanza kurushwa
redioni watu wengi watasikia wengine vitakuwa vinawalenga, hivyo wengine
wataacha na hata serikali ikatatua baadhi ya changamoto ili shule yenu izidi
kuwa salama
Shirika la SUMASESU hivi sasa linatekeleza program ya shule
salama ambapo pamoja na mambo mengine linaandaa vipindi vya redio ambavyo
vinahusiana na shule salama kutoka kwenye maeneo yote ambayo mradi huo
unatekelezwa
No comments:
Post a Comment