Msinitumie kufanya siasa chafu • Nape amjulia hali, azuiliwa kupiga naye picha
Kibanda ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New
Habari (2006) Ltd, alieleza masikitiko yake hayo jana, wakati akizungumza kwa simu na Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Ansbert Ngurumo.
Kauli ya Kibanda inakuja zikiwa ni siku chache tangu mtu aliyejitambulisha kama Ridhiwani Kikwete, atumie ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook kutoa maneno ya kejeli, akihoji kama naye ametekwa na Ikulu.
Kejeli kama hizo pia zilidaiwa kuandikwa katika ukurasa wa facebook wa Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akionesha kufanya propaganda chafu zilizoonesha kama “anawajua” waliomtesa Kibanda.
Katika ukurasa huo wa mtu aliyejitambulisha kama Ridhiwani, aliandika: “Je, hii nayo ni kazi ya Rama (Afisa Usalama wa Taifa) wa Ikulu?”
Rama Ighondu ndiye alitajwa na gazeti la MwanaHALISI kuhusika na mateso ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka Juni 26 mwaka jana.
Kauli hizo zilichefua kwa kiwango kikubwa viongozi wa juu wa Kampuni ya New Habari anayofanyia kazi Kibanda, kiasi cha kumfanya Ofisa Mtendaji Mkuu, Hussein Bashe kuhoji chanzo chake.
Hata hivyo, kwa nyakati tofauti Nape na Ridhiwani Kikwete ambaye ni mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, wamekanusha kuhusika kwa namna yoyote kuandika ujumbe huo wa kejeli.
Katika utetezi wake, Ridhiwani alidai kuwa kuna mtu ameingilia akaunti yake ya mtandao wa kijamii na hivyo kutumia nafasi hiyo kuandika kejeli hizo.
Katika mazungumzo yake na Ngurumo, licha ya kuzungumza kwa shida huku akisikika vizuri, Kibanda alisema kuwa amekerwa na watu wanaotaka kutumia ugonjwa wake kufanya siasa.
“Wanafanya siasa katika hali kama hii? Mambo ya kipuuzi kabisa,” alisema.
Pia alieleza kuwa Nape alifika hospitalini hapo jana asubuhi kumjulia hali.
Hata hivyo, Nape alitaka kupiga picha na Kibanda lakini alikataliwa na walinzi wa hospitalini hapo.
Kuhusu hali ya afya yake, alisema kuwa anasubiri upasuaji wa kuwekewa jicho la bandia baada ya siku 45 kuanzia jana.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika saa 7 alasiri, Kibanda alisema kuwa anasubiri kufanyiwa upasuaji wa pili baada ya jana kurekebishwa uso, taya na meno.
Taarifa ya TEF
Katika taarifa yake kuhusu hali ya afya ya Kibanda, Jukwaa la Wahariri (TEF) lilisema kuwa anaendelea vizuri baada ya upasuaji wa saa 5.30 uliofanyika Jumamosi.
Kwamba Kibanda kulipopambazuka jana alikuwa ameamka na alionekana kupata nafuu kubwa zaidi kuliko ilivyokuwa siku za kwanza.
Sura yake imeanza kurejea katika hali ya kawaida, uvimbe wa damu zilizokuwa zimevilia ndani zimepungua. Hata kuzungumza kwake kuliwatia matumaini wanaomuuguza.
Taarifa hiyo iliyosainiwa na Katibu wa TEF, Neville Meena iliongeza kuwa katika operesheni aliyofanyiwa ni pamoja na ile ya kuondoa jicho la kushoto, pia kurekebisha taya la kushoto.
“Taya hilo pamoja na meno ambayo yalibainika kupata mtikisiko vimefungwa kwa waya maalumu ili kuhakikisha vinarejea katika hali ya kawaida,” alisema.
Kuhusu jicho lililong’olewa, madaktari wanasema wataweka la bandia ambalo hata hivyo halitamwezesha kuona.
Jicho hilo linasubiri uamuzi wa madaktari wanaomtibu ambao walisema wanasubiri kwanza kupona kwa jeraha alilopata.
Meena aliongeza kuwa upasuaji huo aliofanyiwa Kibanda ni wa kitaalamu na haukuhusisha upasuaji wa kutumia kisu (kugusa ngozi yake) bali ni wa kutumia matundu ya pua na kutatua matatizo yaliyokuwa yakimkabili kwa ndani.
Alisema kwa sasa Kibanda anaendelea na matumizi ya dawa kadhaa akiwa chini ya uangalizi wa madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Millpark jijini Johannesburg.
“Kama ambavyo tumekuwa tukihimizana, hiki ni kipindi kigumu katika tasnia yetu ya habari kwa ujumla. Nachukua fursa hii kuwaomba kwamba tuendelee kumwombea mwenyekiti wetu ili Mungu aweze kumponya mapema,” alisema Meena.
Nchimbi akwepa
Katika hatua ya kushangaza, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi jana aligoma kuzungumzia uchunguzi wa sakata la kuvamiwa na kuumizwa vibaya kwa Kibanda, akisema hilo ni suala la ngazi za chini.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari aliouitisha kuzungumzia maofisa waliosimamishwa kazi, Waziri Nchimbi pia aligoma kuzungumzia masuala mbalimbali yaliyoligubika taifa kwa siku za karibuni, likiwemo sakata la Dk. Ulimboka na askari wanaotuhumiwa kupora sh milioni 150.
Badala yake Nchimbi alidai kuwa hayo ni masuala ambayo bado yako ngazi ya chini, kwamba aulizwe Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam, Suleiman Kova na akishindwa ndipo yeye atawajibika kujibu.
Kibanda alivamiwa usiku wa kuamkia Machi 6 mwaka huu, nyumbani kwake Mbezi Beach na kupigwa kwa nondo kichwani kisha kutobolewa jicho la kushoto, kung’olea meno mawili, kukatwa kidole na kunyofolewa ukucha.
Katika hatua ya kuokoa maisha yake, alihamishiwa Afrika Kusini baada ya kupokea matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

No comments:
Post a Comment