Tuesday, March 12, 2013

DIWANI WA KATA ATUHUMIWA KUSHINDWA KUTEKELEZA AHADI YA UJENZI WA BARABARA

Diwani wa kata naye atuhumiwa kushindwa kutekeleza ahadi ya ujenzi wa barabara.

Tofali za kijiji nazo zatelekezwa.
 Afisa mtendaji wa kata ya Utengule amesema kuwa hali ya uongozi  kijiji cha Ngamanga kushindwa kuwasomea wananchi taarifa za mapato na matumizi hadi sasa imepelekea kusimama kwa shughuli za kimaendeleo.
 Tofali zilizotelekezwa kijijini Ngamanga baada ya serikali hiyo kushindwa kutoa taarifa za mapato na matumizi kwa wananchi na hivyo ujenzi kusimama.
 Hizi ni tofali katika kijiji cha Ngamanga ambazo zina miaka mitatu sasa bila kutumika kutokana na kuzitelekeza.
 Diwani wa kata ya Utengule Mh.Erasto Ngota akiwa na afisa mtendajni wa kata hiyo ofisini leo.
 Hii ni bara ya Utengule inayotupiwa lawama na wananchi kwa Mh.Diwani kushindwa kutekeleza ahadi yake ya ujenzi wa barabara hiyo.
Diwani wa kata ya Utengule Erasto Ngota akitoka ofisini kwake mara baada ya kuzungumza na www.gabrielkilamlya.blogspot.com juu ya tuhuma za kushindwa kutekeleza ahadi ya ujenzi wa barabara.

Sakata la Wananchi wa Kijiji Cha Ngamanga Kata ya Utengule Wilayani Njombe Kuikataa Taarifa ya Mapato na Matumizi ya Kijiji Hicho Limeingia Kwenye Sura Mpya,Baada ya Diwani wa Kata Hiyo Kusema Kuwa Hayo ni Matokeo ya Udhaifu wa Uongozi wa Kijiji Hicho.

Akizungumza na www.gabrielkilamlya.blogspot.com Diwani wa Kata ya Utengule Bw Erasto Ngota Amesema Kitendo Cha Wananchi Kuikataa Taarifa Hiyo na Kutishia Kufanya Maandamano ni Ishara Kuwa Uongozi wa Kijiji Umeshindwa Kuongoza Hivyo Wanatarajia Kufanya Mkutano Wiki Ijayo Ili Kuangalia Namna ya Kuuwajibisha Uongozi Huo Ikiwezekana Kuutoa Madarakani.

Amesema Katika Mkutano Huo Wanatarajia Kupokea Mapendekezo ya Wananchi Kama Wanataka Kuendelea na Uongozi Uliopo Madarakani Au Kuubadilisha Kulingana na Namna Uongozi Huo Ulivyosimamia Maendeleo ya Kijiji Hicho

Katika Hatua Nyingine Bw Ngota Amekiri Kuwepo Kwa Malalamiko ya Wananchi Yanayotokana na Kero Mbalimbali Zikiwemo za Ubovu wa Barabara,Ukosefu wa Huduma za Afya za Uhakika na Tatizo la Maji.

Mwishoni Mwa Wiki Iliopita Wananchi wa Kijiji Cha Ngamanga Waliikataa Taarifa ya Mapato na Matumizi ya Kijiji Hicho Ikiwa ni Katika Kile Walichodai Kuwa ni Dosari Kadhaa Zilizopo Kwenye Taarifa Hiyo.

Kufuatia Hali Hiyo Wananchi Hao Waliamua Kuchukua Hatua Mbalimbali Zikiwemo Kufunga Ofisi za Serikali ya Kijiji,Kuwashinikiza Viongozi wa Kijiji Kushiriki Maandamano Yaliotarajiwa Kufanyika Jana Hadi Ofisi za Diwani Ili Kulalamikia Mambo Mbalimbali Yanayoonekana Kuwa Kero Kwa Wananchi Hao

Hata Hivyo Maandamano Hayo Hayakuweza Kufanyika Kutokana na Viongozi wa Kijiji Kutoonekana Eneo la Tukio Hadi Kufikia Majira ya Saa Mbili na Kisha Taarifa Zikaelezwa Kuwa Viongozi Walipata Dharura ya Kuelekea Mjini Njombe Kuhudhuria Semina

No comments:

Post a Comment